Home » » WAPINGA UJENZI WA MAKAO MAKUU KUJENGWA KATA YA TONGWE.

WAPINGA UJENZI WA MAKAO MAKUU KUJENGWA KATA YA TONGWE.


       Na  Walter  Mguluchuma .
           Katavi
  Baadhi ya  Wananchi wa  Tarafa za   Mwese    Karema  wakiwa  na   Madiwani  wao  wanapinga  uamuzi uliotplewa  na   Uongozi  wa  Serikali wa  Mkoa wa  Katavi  wa  kuhamisha   ujenzi wa  makao  makuu ya  Halmashauri  ya  Wilaya ya  Mpanda kwa  sasa  Tanganyika   kutoka   Kata ya  Katuma na  kuhamishia   Kata  ya   Tongwe.
 Wananchi  hao  wamedai  kuwa  kitendo  cha  kuwahamishia  ujenzi wa   makao  makuu ya  Halmashauri yao  kutoka  Kata ya  Katuma    na  kuhamishia   Kata  ya  Tongwe  yanapingana  na  uamuzi wa  kikao  cha    mashauriano   cha    Mkoa wa  Katavi   RCC   kilichoamua  ujenzi wa  makao  makuu ya  Halmashauri  hiyo  kuwa ni Kata ya  Katuma ,
  Diwani wa  Kata ya  Mwese   Juma   Hawazi  akizungumza kwa niaba ya  wananchi wake   mbele  ya  wandishi wa  habari  hapo  jana  alisema  wananchi wa  Kata  hiyo  hawajaridhishwa  wala  kufurahishwa  na   uamuzi  uliotolewa na uongozi wa  Serikali  wa  Mkoa  wa   Katavi  wa  kuhamishia  ujenzi wa   Halmashauri   hiyo     Katika   Kata  ya  Tongwe.
Alisema   lengo  la  Serikali  ni  kusogeza   huduma  karibu  na   wananchi  lakini  eneo  ambalo        limependekezwa  na   Uongozi wa   Serikali  kuwa    makao  makuu ya  Halmashauri  lipo  pembezoni  na  lipo  jirani  sana   na  Halmashauri ya  Manispaa ya  Mpanda na  Nsimbo .
 Alieleza  iliwekwa  tume  maalumu ya watalamu  iliyokuwa   ikifuatilia  ni  eneo  lipi  linalofaa  ambapo  kata ya  Katuma  ilipata   alama   nyingi   na  hivyo  ilipitishwa  na  pia  kikao  cha mwisho  cha  RCC  kilichoongozwa  na  Mkuu wa   Mkoa  mstaafu     Dr   Ibrahimu   Msengi  kilipisha  makao  makuu kuwa   yawe  Kata ya  Katuma .
Mwenyekiti wa  Kijiji   cha   Katuma   Yassin  Kapaya  alisema  wananchi wanajiuliza  na kushangazwa  na taarifa  iliyotolewa   hivi  karibuni  na  Mkuu wa  Mkoa wa   Katavi  Meja  Genelali Mstaafu   Raphael  Muhuga  kuwa  makao  makuu  yatakuwa   kata ya  Tongwe  kata  ambayo  ipo  pembezoni .
 Alisema  wanajiuliza  kama  Rais   alisha   sema  lengo la  serikali yake ni kuwasogezea  huduma  wananchi    ni  vipi  wananchi wa    Halmashauri  hiyo  waendelee  kuwa  mbali  na  huduma .
 Alifafanua   kuwa  wanashangazwa  na sababu  zinazotolewa  na  uongozi wa  Serikali wa  Mkoa wa  Katavi  kuwa    eneo  la    Kata  ya  Katuma  lipo   karibu  na  vyanzo  vya  mto  Katuma  kitu  ambacho  sio  sahihi  kwani  ukweli ni  kwamba    vyanzo vya  mto  vipo  umbali wa kilometa  30  toka   eneo  ambalo   lilipendekezwa  kujengwa  makao  hayo ya  Halmashauri .
 Nae    kiongozi  wa  mila wa  kabila  la   Wabende   Mtemi   Mlela    Malack  alisema  ameshangazwa  na taarifa ya  mabadiliko    hayo   ambayo  ameyaona  kuwa ni  mapya   na yasiyojali  kumsogezea  huduma  mwananchi   karibu
Alisema  anashindwa  kuelewa  vigezo  vilivyotumika   kuhamisha  ujenzi  wa  makao  makuu ya  Halmashauri  kutoka    Katuma   na  kuwa   Tongwe  wakati  Katuma  ndio  katikati  na kuna  njia  za kuingia  na kutoka .
  Mtemi   Malack  alieleza  kama  lengo ni  kusogeza  huduma  kwa  wananchi  yaani  kila  mwananchi  aifuate  huduma   leo  hii  kwanini   Kata ya  Katuma  iliyokatikati   ya    kata  zote  isiwe   makao   makuu  ya   Wilaya  hiyo  mpya  ya   Tanganyika .
Kwa   upande wake   Hamisi  Kiboko alisema kuwa   kitendo cha  kuhamishia  makao  makuu   Tongwe kutaifanya Manispaa ya   Mpanda  kuendelea kubeba  mzigo wa kuwahudumia wagonjwa  kwani  hakuna   mgonjwa  atakae  kuwa  anatoka   Karema    mwese    na   Kabungu  ambae  atakuwa   anakwenda   Tongwe  kutafuta  huduma ya  afya  kulingana  na  jiografia  ilivyo .
   Hivi  karibuni   Mkuu  wa  Mkoa  wa   Katavi   Meja    Generali   mstaafu   Raphael   Muhaga   alitangaza kuwa   makao  makuu ya   Halmashauri  hiyo yatajengwa    Kata  ya   Tongwe  na  kwenye   ziara ya  Waziri   Mkuu  inayoanza   kesho   Mkoani   Katavi   amepangiwa  kutembelea   eneo   hilo .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa