Home » » CHAMA CHA MSINGI CHA MPANDA KATI CHATOWA MSAADA WA DAWATI 100 YA THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 7

CHAMA CHA MSINGI CHA MPANDA KATI CHATOWA MSAADA WA DAWATI 100 YA THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 7

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mkuu wa  Wilaya ya  Mpanda  Paza  Mwamlima akimshukuru mwenyekiti wa  chama cha msingi cha ushirika cha wakulima wa Tumbaku  Mpanda  Kati  Bakari   Hamis  kwa msada uliotolewa na  chama  hicho cha ushirika wa madawati 100 yenye  thamani ya shilingi milioni saba na nusu kwa ajiri ya shule za   msingi wilayani  Mpanda  makabidhiano hayo yalifanyika  jana  katika ofisi za  chama cha Msingi  Mpanda  Kati
PICHA  Na  Walter  Mguluchuma-Katavi yetu Blog
 

  Na  Walter  Mguluchuma
   Katavi
Chama  cha  Msingi cha  ushirika   cha  wakulima   wa Tumbaku cha   Mpanda kati  Mkoa wa Katavi kimetowa  msaada wa   madawati 100   yenye  thamani ya zaidi ya  shilingi milioni saba kwa ajiri ya kusaidia  kupunguza  matizo ya upungufu wa madawati katika  shule za  msingi  katika  Wilaya ya Mpanda.
Msaada huo ulikabidhiwa  jana kwa Mkuu wa  Wilaya ya Mpanda Paza  Mwamlima  katika   makabidhiano yaliofanyika   katika  ofisi za  chama    cha  Msingi   Mpanda  kati  zilizopo  katika  Mtaa wa  Madukani  Mjini  hapa.
Katika  taarifa  iliyosomwa wakati wa kukabidhi  madawati  hayo   na  Meneja wa  chama  hicho cha  ushirika  cha  Mpanda  Kati  Amani   Rajabu  Athuman    mbele ya Mkuu wa  Wilaya ya Mpanda ambae  pia  ni  Kaimu  Mkuu wa  Wilaya  mpya ya  Tanganyika  alisema  chama  hicho kinakabidhi  madawati  100 yenye   thamani ya  shilingi milioni  saba na  nusu.
 Alisema  chama  hicho  kimechangia madawati hayo ikiwa ni  kuunga  mkono juhudi  ambazo  zimekuwa zikifanywa na mkuu huyo wa Wilaya  za kuwahamasisha  wadau   mbalimbali  kuchangia  sekta ya elimu.
Kutokana  na  hamasa  anayoitowa  DC  huyo  ya  kuchangia  madawati   chama  cha  msingi  mpanda  Kati  kitaendelea  kushilikiana  na  Serikali   katika kuchangia maendeleo  kadri uwezo wao.
Meneja  huyo wa  chama  cha  msingi  alieleza  kuwa  mbali ya kutowa msaada huo wa madawati   chama  hicho pia  kimeisha  changia  ujenzi wa  ofisi  ya Kijiji  cha  Majalila, nyumba ya  mwalimu  shule ya Msingi  Mpembe,  na Ujenzi wa   darasa la  shule ya Msingi Igalula
Mkuu wa  Wilaya ya  Mpanda  Paza  Mwamlima  alishikukuru  chamahicho cha Msingi cha Wakulima  wa  Tumbaku  kwa  msada huo na kukiomba  chama  hicho  kiendele kutowa  misaada na  kwenye  sekta  nyingine  kama  afya .
 Alisema  taasisi za   mabenki  zilizopo   katika  mkoa wa Katavi  nazo  zinazo  wajibu wa  kuchangia  mchango wa   madawati  kama  ambavyo walivyofanya  chama  cha  Msingi  Mpanda  Kati .
Nae  Kaimu  Mkurugenzi wa  Manispaa ya Mpanda Lauteli  Kanoni  alisema  madawati  hayo  yatasaidia wanafunzi kusoma  vizuri  shuleni  kwani yatawafanya wasome  shule huku wakiwa wamekaa  kwenye madaw ati.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa