Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Makamu Mwenyekiti wa Taifa Chama cha CHADEMA Tanzania Bara alitejiuzuru Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Said Amour Arfi amewaambia wananchi wa Mji wa Mpanda kuwa uanachama wake katika chama cha CHADEMA utaishia mara tuu baada ya kuvunjwa Bunge la Jamuhuri ya Muungano hapo Julai 9 mwaka huu
Arfi alitowa kauli hiyo hapo jana wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mpanda katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye shule ya msingi Kashato mjini hapa
Pia alitumia mkutano huu kuwaaga Wanachi wa Jimbo la Mpanda Mjini kuwatangazia kuwa hatagombea tena jimbo hilo ambalo ameliongoza kwa kipindi cha miaka kumi
Aliwaeleza wananchi hao kuwa yeye Arfi anatarajia mara ya Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio utakuwa mwisho wake kuwa mwanachama wa CHADEMA kuanzia siku hiyo
Alisema mbalali ya kujiondoa uanachama wake CHADEMA alitangaza kutogombea ubunge wa Jimbo la Mpanda Mjini ambalo amekuwa akiliongoza kwa vipindi viwili kuanzia mwaka 2005 hadi sasa
Arfi alifafanua kuwa yeye hayuko tayari kugogombea jimbo hilo kupitia chama chochote kile cha siasa na kauli hiyo ilemenga kuondoa uvumi uliokuwa umeenea wa kuwa alikuwa na nia ya kugombea kupia ACT au CCM
Alisema amekuwa akishangazwa na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wanachana na wapenzi wa CHADEMA kuwa yeye hajafanya lolote kwenye chama hicho
Kama kuna mtu anae kifahamu vizuri chama hicho basi ni yeye hivyo haoni sababu ya yeye watu kumbeza alikuwa ameamua kukaa kumya hivyo akiamua atamwaga mboga iliwatu wafahamu mapungufu yalioko ndani ya chama hicho
Alisema yeye hagombei jimbo hilo na kama kweli chama hicho kinanguvu basi watetei jimbo hilo ambalo alikuwa analiongoza yeye ila nao uhakika jimbo hilo litakwenda CCM kwani wananchi wa jimbo la mpanda mjini walikuwa na mapenzi na mtu sio chama
0 comments:
Post a Comment