Home » » HOT NEWS: MWALIMU MSTAAFU MWENYE UMRI WA MIAKA 62 KIZIMBANI KWA KUMBAKA MJUU KUU WAKE MWENYE UMRI WA MIAKA MITANO‏

HOT NEWS: MWALIMU MSTAAFU MWENYE UMRI WA MIAKA 62 KIZIMBANI KWA KUMBAKA MJUU KUU WAKE MWENYE UMRI WA MIAKA MITANO‏

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi 
Mwalimu mstaafu wa Shule ya Msingi  Vikonge  Wilayani hapa  Rashiid Mbogo(62) Mkazi wa Kijiji cha Majalila  Kata ya Mpanda  Ndogo  Wilaya ya Mpanda  amefikishwa kizimbani  katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda  kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa maika mitano
 Mtuhumiwa alifikishwa  kizimbani  hapo  jana  mbele ya Hakimu Mkazi  mfawidhi wa mahakama ya  Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa  na kusomewa mashitaka na mwendesha mashitaka Mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi  Naathaniel Silomba
Mwendesha  mashitaka   alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo  hapo Oktoba 19 mwaka huu majira ya  saa mbili usiku  huku akiwa nyumbani kwake
 Mtuhumiwa anadaiwa siku hiyo ya tukio alikuwa amekaa sabuleni akiwa akisubiria  chakula cha  usiku   kilichokuwa  kikiandaliwa jikoni na bibi ya mtoto huyo ambae ni mke wa mtuhumiwa
Mwendesha  mashitaka aliiambia mahakama  wakati akiwa anaendelea kusubilia chakula mtuhumiwa alimwita mjuu kuu  wake sebuleni  na kisha alimweka juu ya mapaja yake na alivua nguo na kuanza kumbaka huku mtoto huyo  akiwa anapiga kelele za kuomba msaada
Mwendesha mashita Silomba aliendelea kuieleza mahakama kuwa  baada ya  kusikia mayowe ya mtoto huyo Bibi  wa mtoto na majirani  waliingia  ndani ya nyumba sebuleni na kukuta mtoto huyo huku akiwa  anatokwa na damu nyingi kwenye sehemu zake za siri na huku akiwa  analia  kutokana n maumivu makali aliyokuwa ameyapata
 Baada ya kusomewa mashitaka hayo mtuhumiwa alikana mashitaka  hayo ambayo alikuwa amesomewa na mwendesha mashitaka
 Hakimu  Chiganga  aliieleza  mahakamani  kuwa mdhamana wa mshitakiwa uko wazi  kwa ajiri ya mdhamana endapo mshitakiwa atamiza mashariti ya mdhamana
Ambapo mshitakiwa alitakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni tano hata hivyo mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti ya mdhamana
Mtuhumiwa alipelekwa rumande ambapo Hakimu Chiganga aliihairisha kesi hiyo hadi hapo Novemba sita itakapo tajwa tena
Yapo makosa ambayo ni makubwa  kama vile wizi wa kutumia silaha , unyang’anyi na kupatikana na dawa za kulevya  adhabu zake ni  k   ndogo kuliko adhabu ya kosa la ubakaji  lakini hayana dhamana huku kosa la ubakaji lenye adhabu kubwa dhamana yake inakuwa ikowazi


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa