Home » » HATARI : MVUVI AKUTWA AMEUAWA NDANI YA NGARAWA PEMBEZONO MWA MTO BAADA YA KUPIGWA NA KITU KINACHO ZANIWA KUWA KIZITO NA WATU WASIO FAHAMIKA.

HATARI : MVUVI AKUTWA AMEUAWA NDANI YA NGARAWA PEMBEZONO MWA MTO BAADA YA KUPIGWA NA KITU KINACHO ZANIWA KUWA KIZITO NA WATU WASIO FAHAMIKA.


Na  Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi yetu Blog
Mtu mmoja mvuvi maarufu wa samaki  aliyefahamika kwa jina la   Credo  Amando (KAMANYOLA) 58  Mkazi wa  Kijiji cha Majomoto   Wilaya ya Mlele Mkoani hapa  ameuwawa baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na mwili wake emekutwa Mvuvi wa samaki  auwawa na watu wasiofahamika  mwili wake wakutwa ukiwa kwenye Ngarawa mtoni 

ukiwa kwenye Ngarawa  pembezoni mwa Mto

Kwa mujibu  ya taarifa aliyoitowa hapo jana  ofisini kweke  mbele ya waandishi wa Habari  na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  tukio hilo lilitokea hapo Agosti  29 mwaka huu majira ya saa saba mchana 

Alisema siku hiyo ya tukio marehemu aliondoka  nyumbani kwake  majira ya saa tatu asubuhi na kuelekea kwenye shughuli zake za kila  siku  za  uvuvi wa samaki kwenye mto  Kavuu ulipo kwenye Kijiji hicho cha Majimoto 

Kidavashari alifafanua  ilipofikia majira ya saa saba mchana wavuvi wenzake waliokuwa wamefika kwenye eneo hilokwa lengo  kuvua samakwaliona Ngarawa pembezoni mwa mtohuku ndani yake  mkiwa na mtu amelala

Alisema wavuvi hao waliamua  kwenda ilipokuwepo Ngarawa hiyo  na ndipo  walipoweza  kuuona mwili wa marehemu Credo  ukiwa ndani ya Ngarawa pembezoni mwa mto  Kavuu huku marehemu akiwa  na majeraha makubwa  sehemu mbalimbali za mwili wake

 Wavuvi hao  walikwenda kutowa taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya Kijiji ambao nao walitowa taarifa kwenye  kituo cha Polisi cha Maji moto ambao walifika kwenye eneo hilo na kisha mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi wa kidakitari na kubaini  kifo hicho kilitokana na marehemu kupingwa na kitu kizito kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake 

Kamanda Kidavashari alisema  katika tukio  hili hakuna mtu wala watu walikamatwa kuhusiana na tukio hili kabla ya kifo hiki  marehemu alikuwa akikorofishana na watu mbalimbali  Kijijni hapo kutokana na tabia yake ya ulevi  uliokithiri wa unywaji wa pombe 

Jeshi la Polisi linaendelea  na upelelezi  wa  kuwasaka  wahusika au muhusika wa tukio hili  kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria  ili sheria  iweze kuchukua  mkondo wake

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa