Tone

Tone

MADIWANI I WA MANISPAA YA MPANDA WATOA TAMKO LA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA HATUA ANAZOCHUKUA ZA KUHAKIKISHA WATANZANIA WANANUFAIKA NA RASILIMALI Z A NCHI ..

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


MZEE WA BARAZA LA MAHAKAMA YA MWANZO JELA MIAKA 3 KWA RUSHWA YA TSHS 50,000.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

JELA MIAKA 20 KWA KOSA LA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO YA MILONI 120.

MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA MALARIA KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Vurugu kubwa zimetokea katika machimbo ya madini ya dhahabu ya Isumamilomo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KATIKA HARAKATI ZA KUCHOTA MAJI KWA AJILI YA MATUMIZI YA SHULE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Wanafunzi wakiwa katika harakati za kuchota maji
 Wanafunzi wakiwa wanangoja kuendelea kuchota maji
Wanafunzi wakiwa wanaenda kuchota maji  
Picha na Walter Nguruchuma Katavi yetu

Vyeti feki vyaathiri huduma Duka la MSD

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. *Lashindwa kufanya kazi saa 24
*Matarajio ya wananchi yatoweka
NA WALTER MGULUCHUMA, Katavi
ILIKUWA ni Jumanne ya Januari 17 mwaka huu pale wananchi wa Manispaa ya Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla walipoyaona mapambazuko ya aina yake katika sekta na huduma ya afya.
Sekta hii muhimu katika maendeleo ya taifa, kwa miaka mingi imekuwa ikikumbana na changamoto kadhaa karibu kila kona ya Tanzania, kubwa ikiwa ni upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.
Jumanne hiyo ya kukumbukwa ndio siku ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozindua duka la serikali linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) lililopo  katika Hopitali ya Manispaa ya  Mpanda  ambayo ndio inayotumika kama  Hospitali ya Mkoa wa Katavi.
Wananchi waliohudhuria hafla hiyo waliifurahia hatua hiyo kutokana na ukweli kwamba mbali na uhaba wa dawa na vifaa tiba kwa mikoa iliyopo pembezoni mwa Tanzania, Katavi ni mmojawapo, tatizo jingine ni ukubwa wa bei za dawa.
“Hili duka la serikali litatuuzia dawa kwa bei tunayoimudu wengi tofauti na maduka ya wafanyabiashara wengine,” alisikika akisema kwa matumaini makubwa mmoja wa wananchi waliokuwapo siku hiyo.
Huenda matarajio na matamanio hayo yakawa yameanza kufifia ndani ya miezi minne tu tangu kufunguliwa kwa duka hilo. Ni nini sababu ya kupungua kwa matumaini hayo?
Serikali ya Awamu ya Tano kwa nia njema kabisa, inaendelea na ukaguzi na ufuatiliaji wa vyeti vya kitaaluma kwa wafanyakazi wake kwenye sekta mbalimbali, ikiwamo pia hii sekta nyeti ya afya.
“Hii ni hospitali kubwa mkoani Katavi; ndio kimbilio letu na haistahili kukosa dawa na vifaa tiba hata vile vya msingi kabisa, lakini bahati mbaya hata bada ya kuwapo kwa dula la MSD, bado tunalazimika kununua dawa kwa wafanyabiashara,” anasema Said Juma, Mkazi wa Kawajense mjini hapa.
Juma anasema Duka la MSD nalo lina matatizo yale yale yaliyopo hospitalini hapo; halina dawa muhimu kwa magonjwa ya kawaida kabisa kwa wakazi wa Mpanda!
“Shida inakuwa kubwa zaidi nyakati za usiku kwani maduka mengi ya dawa huwa yamefungwa. Kimbilio letu huwa ni Duka la Dawa la Mkasu lililo jirani na hospitali. Hapo kila alfajiri utakuta watu walikuwa wakihitaji huduma tangu usiku wa manane, wakisubiri lifunguliwe,” anasema na kuongeza kuwa aghalabu nalo huwa halina baadhi ya dawa walizoandikiwa wagonjwa wengi.
Kukosekana kwa dawa jirani na hospitali, kwa upande mwingine, ni neema kwa waendesha bodaboda wenye kijiwe karibu na Hospitali ya  Mkoa na mmoja wao anasema:
“Watu wengi huwa na haraka ya kununua dawa mbali na hospitali, maeneo ya mjini. Hawa lazima wakodi bodaboda. Hii ndio huduma yetu kwa wananchi na kwetu sisi ni kazi pia.”
Wakati wa uzinduzi wa duka hilo, iliahidiwa kuwa lingefanyakazi saa 24 likiwahudumia wakazi wa Mpanda na mikoa ya jirani.
“Duka hili litamaliza tatizo la upungufu wa dawa katika hospitali hii, vituo vya afya na zahanati za Mkoa wa Katavi. Serikali ina mikakati ya kufungua maduka ya dawa kupitia  MSD kwenye kila mkoa hapa nchini  ili kuondoa  tatizo la vifaa tiba na dawa na kuwapunguzia  wananchi gharama za matibabu,” alisema Majaliwa.
Lakini sasa duka hilo hufanyakazi kwa saa kadhaa tu kwa kuwa hulazimika kufungwa nyakati za usiku kutokana na uhaba wa wafanyakazi.
Walau wafamasia watatu waliokuwa wakihuduma dukani hapo wamekumbwa na zoazoa ya vyeti feki na hivyo kuathiri huduma za duka hilo na kuongeza matatizo zaidi juu ya upungufu uliopo wa dawa dukani hapo.
Wakati wa uzinduzi Januari mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurent Bwanakunu, lengo la kufungua maduka katika mikoa saba nchini ni kusogeza   huduma karibu na wananchi waweze kupata dawa bora na kwa bei nafuu.
Hata hivyo, ahadi hizo za Waziri Mkuu na  Mkurugenzi wa MSD hazijafanikiwa kutatua tatizo la upungufu wa dawa mkoani Katavi.
Kwni  mpaka sasa  dawa  nyingi zimekuwa zikinunuliwa na wananchi kwenye  maduka ya Wafanya biahara wa mitaani kutokana na  duka  hilo la MSD  kutokuwa na  dawa  zenye  mahitaji kwa wananchi.
Baadhi ya  wananchi wameanza kuingiwa na  mashaka kuwa  huenda  ndani zinazoletwa  hapo   ni  zile   ambazo sio  mahitaji kwa  wakazi wa   Mkoa wa  Katavi .
 

MAKALA MUHIMU: NYUMBA YA MKUU WA SHULE YA MSINGI YA MTAPENDA HAINA CHOO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

*Ni katika shule yenye umri wa zaidi ya miaka 40
*Tatizo la maji ya kujisitiri msalani lazidisha kero
NA WALTER MGULUCHUMA, Katavi
Wakati Bunge la Bajeti likiendelea na vikao vyake mjini Dodoma, wadau wa elimu mkoani Katavi wameonekana kusikitishwa na uduni wa mazingira yaliyopo katika shule mbalimbali mkoani hapa.
Katavi ni miongoni mwa mikoa inayofanya vyema katika sekta ya elimu kwa miaka ya karibuni, ikishika nafasi za juu katika matokeo ya jumla ya darasa la saba na hata kidato cha nne.
Lakini nyuma ya mafanikio hayo yanayodaiwa kupatikana kwa jasho la walimu wenye uzalendo mkubwa na kitihada za wazazi na wanafunzi, shule nyingi zimekuwa zikikabiliwa na mazingira duni katika kila hali.

Utafiti uliofanywa na  MWANDISHI WA HABARI HIZI uligundua kuwa moja kati ya shule zenye changamoto zinazoweza kutatuliwa kwa ushirikishwaji kati ya serikali na wadau ni Shule ya Msingi Mtapenda.
Shule hiyo ipo katika Halmashauri ya Nsimbo, Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, ikiwa takriban kilomita 15 tu kutoka mkoani, lakini haina makazi ya walimu na nyumba iliyopo inayotumiwa na Mwalimu Mkuu, haina hata choo.
Shule hiyo ilianzishwa zaidi ya miaka 40 iliyopita wakati Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ilipoendesha Operesheni Vijiji.
Walimu 16 wanaofanya kazi shuleni hapo kwa sasa wote wanaishi katika nyumba za kupanga, nyingi zikikosa hadhi ya kuishi mfanyakazi wa serikali na hivyo wengine kuishi kijiji jirani, wakilazimika kusafiri mwendo mrefu kufika kazini.
“Hata hiyo nyumba anayoishi Mwalimu Mkuu nayo ni majanga tu. Haina choo! Kwa hiyo mwalimu analazimika kuomba msaada kwa majirani kujisitiri. Ni aibu kwa kweli,” anasema mmoja wa walimu wa shule hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Hata hivyo, zipo nyumba (au tuseme mahame) zilizokuwa zimejengwa kwa ajili ya walimu jirani na shule hiyo ambazo kwa hakika ni chakavu kiasi cha kuonekana kama ‘makaburi’ kwa yeyote atakayejaribu kuzitumia, zikiwa zimejengwa kwa udongo.
Mwalimu mmoja aliyejitosa kuishi katika moja ya nyumba hizo anadai kuwa nyakati za mvua huwa hakuna kulala kwani nyumba hizo zinavuja.
“Ni sawa na kukaa chini ya mwembe. Hapo utafurahia kivuli tu lakini mvua ikija, hapafai,” anasema mwalimu huyo.
 Diwani wa Mtapemba, Eliezer Fyula anakiri kulifahamu tatizo la uhaba wa nyumba shuleni hapo, akidai kuwa lipo kwa muda mrefu sasa.
“Hapa tuna bahati kwa kuwa tuna walimu 16, lakini ni bahati mbaya kwamba nyumba zilizoandaliwa kwa ajili yao ni tano tu, nazo ni chakavu kama unavyoziona.
“Ni moja tu ndio imejengwa kwa matofali ya kuchoma, nyingine ni matofali ya udongo tu. Wenyewe wanaita biskuti. Zipo katika hali mbaya sana,” anasema Fyula.
Anasema tatizo hilo linachagizwa na Halmashauri ya Nsimbo kutotenga fedha kwa ajiri ya ujenzi wa nyumba za walimu licha ya yeye kuishauri mara kwa mara.
Kwa upande mwingine, katika Kijiji cha Majimoto wilayani Mlele, tatizo la maji lililopo maeneo hayo husababisha hata wanafunzi kushindwa kuendelea na ratiba ya masomo kama ilivyopangwa.

Katika Shule ya Msingi Majimoto,  MWANDISHI WA  HABARI HIZI  iliwashuhudia watoto wakitoka madarasani kwenda kutafuta maji kwa ajili ya matumizi, hasa ya chooni, kwani shule haina kisima wala bomba la maji.
Wakizungumza na mwandishi wetu, wanafunzi hao waliokuwa wakichota maji katika chemchem maarufu inayotoa maji ya moto, walilalamikia hali hiyo.
“Shuleni hakuna huduma yoyote ya maji na kama kusingekuwapo chemchem hapa karibu, sijui tungepata wapoi maji. Kila mara huwa tunakatisha masomo kuja kuchota maji,” anasema mtoto mmoja wa darasa la tatu.
Ni kawaida kwa kila mwanafunzi anayesoma shuleni hapo kuwa na dumu (kopo la plastiki) la lita tano kwa ajili ya kuchotea maji kwenye chemchem hiyo.
Jina la kijiji, Majimoto, linatokana na kuwapo kwa chemchem hiyo inayotoa maji ya moto kiasi cha kulazimika kuyapoozesha kabla ya kuyatumia. Maji hayo hutiririka kwa mwaka mzima.
Hata hivyo, maji hayo yanayotokana na nguvu za asili (volcano), hayafai kwa kunywa.
“Tumeshazoea kwa sababu imekuwa kawaida kabisa kuja kuchota maji hapa. Tutfanyaje na chooni hakuna maji? Ni lazima kila sku kuja hapa kuchota maji,” anasema binti huyo.

Pamoja na kufahamu kwamba maji ya chemchem hiyo hayafai kwa kunywa, MWANDISHI iliwashuhudia watoto kadhaa wakiyanywa baada ya kupoa, wakisema hawana sehemu nyingine ya kupata maji ya kunywa.
Kwa ujumla maji ni tatizo kubwa kijijini hapo na wananchi husafiri kwa takriban kilomita sita kufuata maji katika Kijiji cha Mamba.

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJARIWA AFUNGUA DUKA LA DAWA MKOANI KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri Mkuu Mh. Kassim Majariwa akikata utepe kuashiriwa kuzinduliwa rasmi kwa Duka hilo.
Waziri  Mkuu Mh. Kassim Majariwa (wa kwanza Kushoto)  akimsalimia mmoja wa akina  mama  wajawazito katika wodi no 4  kabla ya kuzindua duka la  dawa la msd katika  hopitali ya  manispaa ya mpanda inayotumika kama hospitali ya  mkoa wa katavi 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa