Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kasokola katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Jonas Msusa amevamiwa na majambazi wakati alipokuwa amelala nyumbani kwake usiku wa manane kwa kushambuliwa na silaha za jadi na kujeruhiwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kupolwa kiasi cha zaidi ya Tshs 500,000.
Tukio hilo la kuvamiwa na kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Chama hicho cha msingi cha ushirika wawakulima wa tumbaku lilitokea hapo juzi majira ya saa nane usiku nyumbani kwake katika Kijiji cha Kasokola Wilayani Mpanda .
Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho Dominick Fungameza alieleza uwa siku hiyo ya tukio Jonas Msusa alikuwa amelala nyumbani kwake na familia yake ndipo walipotokea majambazi hao na kuvunja mlango na kisha waliingia moja kwa moja hadi kwenye chumba alichokuwa amelala na mkewe.
Alisema baada ya kuingia ndani ya chumba majambazi hao waliukuwa wanne walianza kumshambulia katika sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia silaha za jadi fimbo ,malungu na kisu .
Wakati wakimshambulia mwenyekiti huyo mkewe alikuwa akishuhudia kitendo hicho na alitakiwa na majambazi hao asipige mayowe na endapo angepiga mayowe walimtishia kuwa wangemuua.
Alisema baada ya kumshambulia na kuona amepoteza fahamu walipekua kwenye nguo zake alizokuwa amevaa mchana na ndipo walipoweza kufanikiwa kuchukua fedha kiasi cha Tshs 550,000 zilizokuwa kwenye suluale yake na kisha walitokomea kusiko julikana .
Majirani walifika kwenye eneo hilo na walimkuta Jonas Msusa akiwa anagalagala chini ya sakafu huku akiwa amepoteza fahamu na sehemu za mwili wake zikiwa na majeraha mbalimbali na ndipo walipomkimbiza kwenye Hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambako amelazwa akiendelea kupatiwa matibabu .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hili Jonas Msusa huku akiwa amelazwa katika wodi ya Bima ya Afya katika Manispaa ya Mpanda alisema majambazi hao alisema kabla ya kuwa amepoteza fahamu aliweza kupambana nao kwa zaidi ya dakika 15 na ndipo walipoweza kumzidi nguvu.
Alisema siku hiyo ya tukio mchana wake alifanya kazi ya kuongoza kikao cha mkutano mkuu wa chama cha Msingi cha ushirika wa wakulima wa tumbaku Kasokola hivyo anahisa kuwa majambazi hao walidhani kuwa alikuwa na fedha za chama hicho .
Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limethibitisha kutokea kwa tukio la kuvamiwa na kupolwa kwa mwenyekiti huyo na hakuna hadi sasa mtu yoyote alikamatwa kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment