Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanazuia dawa za binadamu hazitoroshwi kwa njia za panya kwenda Nchi za jirani na zile dawa haramu na vipodozi vinavyoingizwa vinavyoingizwa nchini kwa njia haramu .
Naibu Waziri alitowa agizo hilo hapo jana wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake ya siku tatu Mkoani hapa .
Alisema Serikali imeongeza bajeti ya ya kununua dawa kutoka shilingi Bilioni 30 hadi kufikia shilingi Bilioni 270 zikiwa ni mara tisa zaidi kwa lengo la kuboresha zaidi huduma za afya kwa wananchi .
Pamoja na jitihada hizo za Serikali za kuboresha huduma za afya kwa kuongeza bajeti hiyo imekuwa ikiwanufaisha baadhi ya watu wa nchi za jirani kutokana na watu kutorosha dawa kwa njia za panya . na kwenda kuziuza huko .
Alisisitiza kuwa Serikali haiko tayari kuona wala kusikia wananchi wake wanakosa dawa badala yake watu wa nje ya Nchi ndio wanaonufaika na dawa hizo zinazonunuliwa na Serikali ya Tanzania .
Alisema kutokana na hari hiyo anaiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Katavi kuhakikisha dawa zinazonunuliwa na Serikali havivushwi kwenda nchi za jirani wala kuruhusu dawa haramu na vipodozi kuingia hapa Nchini kwa njia haramu .
Alisema Wizara ya Afya imejipanga hukakikisha Hositali za Mikoa inazisimia ilizitowe huduma vizuri na pia imeandaa utaratibu wa kuvizawadia vituo vyote vya afya ambavyo vitakuwa vimefanya vizuri . katika kutowa huduma bora na nzuri.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphaeli Muhuga alimwakikishia Naibu Waziri kuwa endapo tatizo hilo kama lipo watalifatilia na kulishughulikia mara moja.
Pia alisema Mkoa wa Katavi unakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na Hospitali ya Mkoa na badala yake Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ndio inayotumiwa kama hositali ya Mkoa na kwagharama ya Bajeti ya Manispaa ya Mpanda hari ambayo inaifanya Hositali hiyo kuelemewa na mzigo .
Aliitaja changamoto nyingine kuwa ni Halmashauri za Mkoa huo kutokuwa na Hositali zao ambapo katika Halmashauri tano zilizopo katika Mkoa huu ni Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda peke yake ndio inayo Hositali .
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Yahaya Hussein alieleza kuwa Mkoa umeendelea kuongeza bajeti ya dawa ili kuhakikisha kuwa huduma za dawa zinapatikana katika ngazi zote za kutolea huduma .
Alifafanua kuwa kwa mwaka 2012 bajeti ya Mkoa ya dawa na vifaa ilikuwa ni shilingi 558,000,000.00 ambayo kimsingi ilikuwa haitosherezi mahitaji ya dawa na vifaa tiba ,ukilinganishwa na bajeti ya mwaka 2017/ 2018 ambapo Mkoa umetengewa jumla ya shilingi Bilioni 2,917,363,715,00 ambayo wanaamini itaongeza upatikanaji wa dawa , vitendanishi na vifaa tiba kutoka asilimia 54 hadi 93.
MWISHO
No comments:
Post a Comment