Na Walter Mguluchuma.
kATAVI
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa (CCM)
wa Wilaya ya Mpanada mkoani Katavi Beda Katani amechaguliwa
kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Katavi baada ya kushinda
mgombea mwenzake kwenye nafasi hiyo Enock Gwambasa ambae aliwahi
kuwa meya wa Manispaa ya Mpanda .
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi , Deo Njinjimbi alimtanga Katani kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Katavi baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa wa katavi uliofanyika jana na matokeo kutangazwa jioni mjini Mpanda.
Katika uchaguzi huo Beda
Katani ” alipata kura 304 , huku mpinzani wake Enock Gwambasa
akipata kura 46 nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa CCM wa Katavi
ilikuwa na wagombea wawili tuu .
Mkutano
huo Mkuu wa CCM wa Mkoa ulimchagua pia Gilbelti Sampa kuwa
mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM NEC baada ya kuwashinda
wagombea watatu wanafafi hiyo .
Sampa
alishinda baada ya kupata kura 182, na wagombea wenzake
walipata Wense Ka mtoni kura , 157, Hassanal Dalla kura 66 na
Alkado Kalifumu kura 4.
Aidha Halmashauri Kuu wa CCM mkoa wa Katavi ikiongozwa na mwenyekiti wake mpya , Beda Katani ilimchagua Jackoson Lema kuwa Katibu Mwenezi CCM mkoa wa Katavi ambaye alifanikiwa kupata kura 24. na kumshinda mgombea mwenzake Linus Kasakabaya alipata kura 12.
Katika hotuba yake mbele ya wajumbe wa Mkutano mkuu
Mwenyekiti huyo mpya wa ccm aliwahakikishia wajumbe hao kuwa
atahakikisha anafanya kazi ya kuimarisha chama hicho pasipo
kuwa na ubaguzi wowote na muda wote atakuwa yuko tayari kwa ajiri
ya kusikiliza kuro za watu na kuzipatia ufumbuzi wake .
Mkoa wa Katavi ambao ulianzishwa mwaka 2012 hivyo Beda Katani
amekuwa ni mwenyekiti wa pili wa chama hicho toka Mkoa wa
Katavi ulipoanzishwa Mwenyekiti wa kwanza alikuwa ni Mselemu
Abdala ambae kwenye uchaguzi huu hakugombea.
MWISHO
No comments:
Post a Comment