Na Walter Mguluchuma.
Mlele Katavi
Mlele Katavi
MKAZI wa Sumbawanga mjini mkoa Rukwa , Raphael Kusa (18) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi akishtakiwa kwa makosa manne ya uhujumu uchumi ikiwemo kukutwa na nyara za Serikali zenye thmani ya zaidi ya Sh milioni 3.0
Mshtakiwa huyo alifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Tiotemus Swai wa Mahakama ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi ambapo hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa makosa yote manne yameagukia kwenye makosa ya uhujumu uchumi ambapo mahakama hiyo haina malaka ya kuisikiliza ilisipokuwa Mahakama Kuu .
Kusa anashitakiwa kwa makosa ya kukutwa na bunduki aina ya gobori , vilipuzi vyenye nuzito wa gramu 200 na risasi 21 za gobori bila kuwa na kibali halali ambapo ni kinyume na Sheria ya uthibiti wa silaha na risasi kifungu cha sheria namba 20(1) (2) ikisomwa pamoja na Sheria ndogo namba 2 ya 2015 ya uhujumu uchumi .
Pia nashtakiwa kwa mujibu wa Sheria ya milipuko kifungu cha Sheria namba 11(1) ikisomwa pamoja na Sheria namba 3 ya 2016
Pia alikuwa nyara za Serikali ukiwemo mkia wa nungunungu wenye thamani ya Sh 336,000/- na mikia miwili ya mnyama pori aitwae pongo kwa jumla ikiwa na thmani ya Sh 1,344,000/-ikiwa nikinyume cha Sheria namba 5 ya 2009 , kifungu cha 86(1) (2) (b) (II)
Swai aliamuru mshtakiwa kurejeshwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana huku akiiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 22 , mwaka huu itakapotajwa tena .
Awali Mwendesha Mashtaka , Mkaguzi wa Polisi , Baraka Hongoli alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Desemba 03, mwaka huu ndani ya Pori la Hifadhi la Rukwa – Lwafi wilayani Mlele mkoani humo .
Mwisho
No comments:
Post a Comment