Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu Lazaro Peter Ngomalala 50 Mkazi wa Kijiji cha Simbwesa Wilaya ya Tanganyika kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka tisa jina limehifadhiwa mwanafunzi wa darasa la pili wa Shule ya Msingi Simbwsa.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashitaka akiwemo mwanafunzi huyo aliyebakwa uliotplewa Mahakani .
Kabla ya kutowa hukumu hiyo Hkimu Ntengwa alisema mtu yoyote anaefanya kitendo kama alichofanyiwa mtoto huyo anakuwa amrfanya kosa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 130 kifungo kidodo cha kwanza na cha pili na na kifungu cha sheria namba 131 kifungu kidogo cha tatu cha kanuni ya adhabu .
Alieleza kutokana na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka akiwemo mtoto mwenyewe na mtoto mwenzake ambae alishudia tukio hilo Mahakama pasipo shaka yoyote imemwona mshitakiwa Lazaro Ngomalala kuwa anayohatia .
Ntengwa alisema miuongoni mwa ushahidi wa sababu zilizoifanya Mahakama imtie mshitakiwa hatiani ni ushahidi uliotolewa mahakani na mtoto alibakwa na mtoto mwenzake mwenye umri wa miaka saba licha ya kuwa na umri mdogo walitowa ushahidi kwa ufasaha mkubwa juu ya tukio hilo.
Pia Mahakama ilijiridhisha na ushahidi uliotolewa na muuguzi wa Zahanati ya Simbesa alimfanyia uchunguzi na kubaini i kuwa mtoto huyo alikuwa amembakwa hari ambayo ilimlazimu muuguzi huyo amwanzishie dawa ya kuzuia maambukizi ya VVU.
Kabla ya kusomewa hukumu hiyo hakimu Ntengwa alitowa nafasi kwa mtuhumiwa Lazaro kama anayosababu ya msingi ya kuishawishi mahakama iweze kumpunguzia adhabu hivyo mshitakiwa aliiomba Mahakama imwachie huru kwa kile alichodai kuwa yeye hakutenda kos hilo bali amesingiziwa na mama mzazi wa mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimdai fedha alizokuwa anamdai baada ya kumkopesha.
Baada ya utetezi huo wa mshitakiwa Hakimu Chiganga Ntengwa alisema kutokana na mshitakiwa kupatika na hatia ya kifungu cha sheria namba 131 kifungu kidogo cha cha tatu kinachoeleza mtuyoyote atakae mbaka mtoto mwenye umri wa chini ya miaka kumi adhabu yake ni kifungo cha maisha jela .
Hivyo kutokana na mshitakiwa Lazaro Ngomalala kupatikana na kosa hilo Mahakama imemuhumu kuanzia jana kutumkia jela kifungo cha maisha jela .
Awali kwenye kesi hiyo Wakili wa Serikali Fravian Shiyo alidai Mahakamani hapo kuwa Lazaro alitenda kosa hilo hapo Oktoba 12 mwaka jana majira ya saa nne asubuhi kijiji katika Jijiji cha Simbesa.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio mshitakiwa alikuta mtoto aliyemtenda kitendo hicho akiwa na mtoto mwenzake wakiwa wanacheza jirani na nyumba yao ndipo alipowadanganya wafuate nyumbani kwake iliakawapatie fedha za kununulia biscuit na soda .
Shiyo alieleza kuwa wakati wakiwa wanaelekea nyumbani kwa mshitakiwa walipofika kwenye eneo la tanki la maji Lazaro alivuta kwa nguvu mtoto huyo na kuanza kumbaka licha ya mtoto huyo kubiga kelele lakini hakuweza kumwachia mpaka alipo maliza aja yake .
Mwanasheria aliiambia Mahakama baada ya kufanyiwa kitendo hicho mtoto huyo alibakwa alikwenda kutowa taarifa kwa wazazi wake huku akiwa analia na baada ya kutowa taarifa kwa wazazi wake mtuhumiwa alikamatwa na askari wa mgambo wa kijiji cha Simbwesa na kisha alifikishwa katika kituo cha polisi
MWISHO
No comments:
Post a Comment