Na Walter Mguluchuma.
Katavi
MAMLAKA ya Wanyamapori Tanzania TAWA imefanya doria kudhibiti
ujangili na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 3,185 na kesi 1,539
zilifunguliwa mahakamani katika kipindi cha Julai Mosi mwaka jana
hadi sasa .
Katika kipindi hicho washtakiwa 463 wainusurika vifungo baada ya
kulipa faini ya zaidi Sh milioni 450/.
Kaimu Mkurugenzi wa TAWA , Martin Loibook alieleza mafanikio hayo
wakati wa ufungaji rasmi wa mafunzoya wiki sita yaliyohudhuriwa
maofisa wanyamapori 97 kutoka TAWA
yaliyofanyika katika Kituo cha Mafunzo ya ukakamavu kilichpo katika
Pori la Akiba la Rukwa Lwafi lililopo katika wilaya ya Mlele mkoani
Katavi .
Mafunzo hayo ni kwa ajili ya maandalizi ya kuingia katika mfumo wa
Jeshi Usu kutoka mfumo wa uraiani ambayo yameenda sambamba na Tawa
kumaliza mwaka mmoja tangu ilipoanza kufanya kazi rasmi Julai Mosi
mwaka jana .
Alisema katika kipindi hicho TAWA iliweza kufanya siku za doria
147,169 za kudhibiti ujangili ambapo silaha 270 zilikamatwa
zikiwemo SMG 22, bastola mbili bunduki za uindaji aina ya rifle 47 ,
shot gun 21 magobori 178 na risasi 1,058.
Aliongeza kuwa katika kuimarisha ukaguzi wa nyara za Serikali
katika vituo vya mipakani na viwanja vya ndege raia wakigeni wapatao
29 walikamatwa kwa makosa ya kutorosha nyara za Serikali nje ya
nchi ambapo kesi 25 zilifunguliwa katika vituo vya polisi na
zlikamilika kwa watuhumiwa kulipa faini y zaidi ya Sh milioni 43 .
Alisema katika kipindi hicho meno ya tembo mazima 129 na vipande 95
vilikamatwa kwa pamoja nyara hizo zilikuwa na uzito wa kilo 810.3.
Aidha, Machi mwaka huu raia wawili wa kigeni walikamatywa a kobe
hai 171 katika matukio tofauti yaliyotokea Dar Es Salaam na Njombe
.
Alizitaja changamoto kadhaa ikiwemo uvamizi wa mifugo hifadhini ,
migogoro ya mipaka , kuingizwa nchini silaha za kivita zinazotumika
kufanya visa vya ujangili na kurudishwa kwa vitalu vya uwindaji wa
kitalii kutokana na uvamizi wa mifugo na uelewa mdogo wa wananchi
katika kuunga mkono uhifadhi wa rasilimali za maliasili.
Kwa upande wake Katibu |Mkuu wa Wizara yaMaliasilli na Utalii , Meja
Jenerali , Gaudensi Milanzi aliwataka wahifadhi wote kwa kushirikiana
na mamlaka za mikoa na wilaya kuhakikisha t.atizo la uvamizi wa
mifugo hifadhi ni linamalizika .
Aliwataka wananchi kuheshimu sheria za nchi na kuacha kufanya
shughuli za kibinadamu hifadhini .
Mwisho
No comments:
Post a Comment