Na Walter Mguluchuma.
Katavi
Mahakama ya wilaya ya Mlele imemuhukumu mlinzi wa shule ya
Sekondari Ilela iliyopo wilayani humo, George Sikoki kutumikia kifungo
miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa umri wa
miaka 16.
Hukumu hiyo imetolewa juzi na Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo,
Teotimus Swai baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani
hapo.
Awali, Mwendesha Mashtaka mkaguzi wa Polisi, Baraka Hongoli alisema
mahakamani hapo kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 27 mwaka
huu nyakati za saa 7:30 usiku.
Aliieleza mahakama hiyo kwamba, Sikoki ambaye ni mlinzi wa shule ya
sekondari Ilela iliyopo tarafa ya Inyonga wilayani humo, alisikia
kwamba wazazi wa mtoto huyo wamesafiri hivyo mtoto huyo ana lala peke
yake, hivyo usiku huo alikwenda nyumbani kwa mtoto huyo na kuvunja
mlango kisha kumtishia kumuua mtoto huyo iwapo atapiga kelele hivyo
kumbaka na kutokomea kusikojulikana.
Alisema kuwa binti huyo akiwa na maumivu makali huku akitokwa na damu
sehemu za siri alijingongoja hadi kwa jirani na kutoa taarifa kisha
kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Mwendesha mashitaka Hongoli aliendelea kuieleza mahakama kwamba baada
ya mtuhumiwa kukamatwa alikiri kosa hilo kwa maandishi wakati
akihojiwa kituo cha polisi lakini alipofikishwa mahakamani alikana
shitaka hivyo mahakama kuitaji ushahidi ambapo upande wa jamhuri
ulipeleka mashahidi sita akiwemo daktari alithibitisha kubakwa kwa
mtoto huyo.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Swai alidai kwamba pasipo na shaka
mahakama imebaini kwamba mshitakiwa amekutwa na hatia hivyo kwa
kuzingatia vifungu sheria namba 130 (1) (2) E na 131 1 anahukumiwa
kwenda jela miaka 30.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment