Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge kazi, ,Ajira Kazi .vijana na watu wenye ulemavu Jenista Mhagama amewataka vijana hapa Nchini kutumia sekta ya kilimo na sekta isiyo rasmi ili kukuza uchumi wa Nchi na uchumi wao.
Mhagama alitowa kauli hiyo hapo jana wakati alipokuwa akifungua kongamano la vijana lililofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi na liliwashirikisha vijana 150 kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi .
Alisema endapo vijana ambao ndio nguvu kazi ya Nchi hii watatumia vizuri sekta ya kilimo na sekta isiyo rasmi zitawasaidia kubadili maisha yao na kukuza uchumi wa ncihi kwani sekta isiyo rasmi na kilimo ndizo ambazo zinawagusa vijana wengi .
Alisema vijana wa Mkoa wa Katavi wanayo kazi kubwa ya kujenga uchumi wa Mkoa wao na uchumi wa Nchi kwani vijana hapa nchini wanachangia asilimia 55 ya nguvu kazi ya Taifa .
Waziri Mhagama alieleza Serikali imeamua kuweka mkazo wa kukuza ujuzi wa vijana wa Nchi yetu kwa kuwatowa kwenye ujuzi mdogo ili waweze kwenda kwenye uchumi wa kati .
Alifafanua kuwa viwanda vidogo na viwanda vya kati ndivyo ambavo vitategemewa sana katika swala la kukuza uchumi wa Nchi katika nchi nyingi duniani .
Alisema Serikali itaendelea kuboresha mifuko ya mikopo ya vijana ili kuboresha uchumi wa vijana na itatowa mikopo kwa miradi iliyo na tija na miradi ambayo haina tija Serikali haitatowa mikopo .
Hivyo vijana wafanye kazi kwa bidii na wawe wavumilivu na wajiendeleze kwenye sekta za kuwaletea maendeleo kwa kuanzisha vikundi vya kuwaletea maendeleo .
Aliwaonya vijana waache kupenda maendeleo ya haraka kwa kutumia kwa njia ya mkato na badalala ya kufanya kazi kwa bidii na kupata maendeleo yao kwa hatua kwa hatua .
Alisema vijana wengi hapa Nchini hawapendi kufanya kazi na badala yake wanapenda utajiri wa haraka haraka bila kufanya kazi .
Pia amewataka vijana kuwa wapambanaji wa kupambana na kurushwa , dawa za kulevya na ugonjwa wa ukimwi kwani wao bila kutowa ushirikiano kwa serikali haitaweza kufanikiwa .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhaga alisema kongamano hilo la vijana litawasaidia kuzifahamu rasilimali zilizopo katika Mkoa huo na watapata nafasi ya kuelishwa namna ya kuunda vikundi vya ujasiliamali na jinsi ya kukopa katika taasisi za kibenki.
MWISHO
No comments:
Post a Comment