Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Viongozi wa wa Chama cha Msingi cha ushirika cha Wakulima wa Tumbaku cha Mpanda Kati wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa wa kufanya shuguli za ushirika kwa ufanisi zaidi na kujua makumu yao.
Msimamizi na mdhibiti wa vyama vya Ushirika wa Mkoa wa Katavi Gabinus Msonga alisema mafunzo hayo ya siku kumi yaliwashirikisha wajumbe wa Bodi hiyo ya ushirika ya Chama cha Msingi Mpanda kati yalifungwa jana katika ofisi za chama hicho katika Mtaa wa Madukani
Alisema kwa sheria ya ushirika namba 6 ya mwaka 2013 inaeleleza kuwa wajumbe wote wa bodi ya vyama vya Msingi vya ushirika wa Tumbaku wanapo kuwa wameingia madarakani ni lazima wapatiwe mafunzo hayo .
Alifafanua kuwa wajumbe wa bodi hiyo toka walivyoingia madarakani wamefikisha kipindi cha mwaka mmoja sasa na walikuwa hawajapatiwa mafumzo hayo hali ambayo imekuwa ikipekekea baadhi ya mambo kutokwenda sawa kutokana na wajumbe hao kutokuwa na uwelewa wa majukumu yao /
Mtonga alieleza mafunzo kama hayo yamefanyika katika vyama vya Msingi vya wakulima wa Tumbaku vya Msingi vinne ambavyo ni Mishamo Amcos, Okonongo na Mishamo Tamcos na mafunzo hayo yamekuw yakitolewa na maafisa ushirika wa kutoka Wilaya za Mpanda na Mlele.
Alisema ilikuwa na vyama vya Msingi vyenye nguvu vya wakulima wa Tumbaku katika Mkoa wa Katavi ofisi ya Ushirika ya Mkoa imeisha weka utaratibu wa kutokubali kuanzishwa kwa vyama vya msingi ambavyo sio endelevu .
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Edga Mpendakazi alisema mafunzo hayo waliyoyapata yatawasaidia kuongeza uwezo wa kufanya shughuli zao vizuri zaidi kwani walikuwa wakifanya shughuli bila kuwa na ufahamu wa kujua majukumu yao .
Pia yamewaongezea uwezo wa ulimu ya kuwaelisha wanachama wao wanaowaongoza namna ya kuwajengea uwezo wa kukuza uchumi wao na kukuza kipata cha wanachama .
Makamu Mwenyekiti wa Bodi wa Bodi ya chama cha ushirika cha Msingi Mpanda Kati Onerati Yamini alisema mafunzo hayo yamewapatia mwanga w kukiongoza chama chao cha Msingi .
Alisema pamoja na bodi hiyo kutokuwa na elimu hiyo walioipata bodi hiyo iliweza kufanikiwa msimu uliopita kuwalipa wakulima wake malipo ya mauzo ya wanachama wao kwa asilimia mia moja tofauti na wajumbe wa bodi waliokuwa wametengulia ambapo hawakuweza kulipa malipo kwa asilia hizo .
Mjumbe wa Bodi Moshi Kalele alisema wamekuwa wakikabiliwa na baadhi ya changamoto mbalimbali baadhi ya changamoto hizo ni kuchelewa kuisha kwa msimu wa ununuzi wa masoko ya Tumbaku hari ambayo imekuwa ikisababisha chama hicho kuingia gharama .
mwisho
No comments:
Post a Comment