Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge , Kazi,Vijana Ajira na Watu wenye ulemavu Jenista
Mhagama aliyekatika kati akiwa na Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga pamoja na
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda..
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali
Mstaafu Raphael Muhuga akimwongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera Bunge ,Kazi Vijana Ajira na Watu wenye
ulemavu Jenista Mhagama kukagua uwanja unaojengwa ambao
zitafanyika shughuli za uzinduzi wa mbio za Mwenge Mkoani
Katavi hapo Aprii 2 2017
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge Kazi , Vijana ,Ajira na Watu mwenye ulemavu
akikagua uwanja mpya unaojengwa Mkoani Katavi katika eneo
la Mtaa wa Ilembo Manispaa ya Mpanda unaitwa Mwenge ambao
ndio utakaotumika kwa ajiri ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa
Uhuru hapo Aprii 2/ 2017
Picha zote Na Walter Mguluchuma Katavi yetu Blog
Walter Mguluchuma na Irene Temu
KATAVI
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh.Jenista Mhaga
ameupongeza Mkoa wa Katavi kwa maandalizi mazuri ya uzinduzi wa mbio za
mwenge wa Uhuru unaotarajia kuanza mbio zake April 2 mwaka huu na mbio
hizo zitazinduliwa Mkoni Katavi.
Akizungumza na viongozi mbalimbali wa serikali wa Mkoa huo na Waandishi wa Habari hapo jana katika
Ukumbi wa Ikulu ndogo iliyopo Mkoani hapo,Waziri Jenista ameipongeza
kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio hizo za mwenge wa Uhuru ambao
utazinduliwa katika Uwanja uliopewa jina la Mwenge mnamo tarehe 2 mwezi
wanne mwaka huu kwa maandalizi mazuri na kusema serikali imeipa Mkoa wa
Katavi heshima ya kuzinduzia mbio hizo za Mwenge wa Uhuru ili
kuhakikisha unachochea maendeleo Mkoani hapo.
Pia Waziri Jenista alisema“Mwenge wa Uhuru
kuzinduliwa mkoani Katavi kutaupa nafasi Mkoa wa Katavi kujitangaza
ndani na nje ya nchi na kuchochea maendeleo,kutangaza fursa za kiuchumi
na rasilimali zilizopo ndani ya Mkoa.
Alifafanua kuwa falsafa ya Mwenge imeasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere mnamo tareha 9 mwezi Disemba mwaka 1961 siku ya Uhuru
Sambamba na hayo Waziri Mhagama alikumbushia kuwa
kila mwaka katika uwashwaji wa mwenge huwa kunakuwa na kauli mbiu
ambapo ujumbe wa mwaka huu unasema“Shiriki katika uchumi wa viwanda kwa
maendeleo ya nchi yetu”
Aidha Waziri ameeleza kuwa serikali itaendelea kutangaza ujumbe mwingine wakati wa mbio za mwenge ili kuhakikisha inapinga rushwa na ndio maana imekwisha kufungua mahakama ya kupambana na rushwa na pia kupiga vita madawa ya kulevya lengo likiwa ni kuwaokoa vijana ili waweze kufanya kazi na kupambana na Ukimwi na Malaria.
Mwenge wa uhuru utakimbizwa katika mikoa yote 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na halmashauri195 zilizopo hapa nchini na kutimishwa kilele chake Oktoba 14 mwaka huu Mjini Magharibi sambamba na kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Julius Nyerere
Alikemea tabia ya watu wanaoeneza kuwa mwenge wa uhuru ni wa chama cha siasa hivyo watu wanapaswa watambue kuwa mwenge wa uhuru si wa chama cha siasa bali ni wa watanzaniz wote.
MWISHO
No comments:
Post a Comment