Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na wadau wa ulinzi na usalama na mamlaka ya kukusanya mapato TRA wamewakamata watu 16 kati yao wanawake watatu wakiwa na Katoni 1364 za pombe za aina mbambali za viroba vyenye thamani ya shilingi milioni 99,871,000.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda aliwaambia wandishi wa Habari jana kuwa watuhumiwa hao 16 walikamatwa kufuatia msako uliofanyika siku mbili za Machi 6 na Machi 7 katika maeneo ya Manispaa ya Mpanda .
Alisema Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi lilifanikiwa kuwakamata watu hao kufuatia msako mkali waliofanya kwa kushirikiana na TRA ,Mamlaka ya chakula na dawa na TAKUKURU.
Kamanda Nyanda alieleza katika msako huo umbao ulifanywa katika maduka ya jumla na kwenye mabaa na kwenye maeneo mengine pia waliweza kukamata katoni 362 za pombe za viroba aina ya Boss nyenye thamani ya Tsh s milioni 29,000 vikiwa vimebebwa kwenye gari aina kenta yenye Namba za usajiri T 498 clz mali ya Hery Ngiza mkazi wa Mkoa wa Mwanza .
Kamanda Nyanda alitaja ina ya viroba vilivyo kamatwa kuwa ni Boss katoni 362, Value Katon Katon 28, Konyagi katoni 62,Zed katoni 473 Zanzi katoni 25 Londoni 400, cinja,11 Highlifegin ,Dalious21 na Leared.
Alisema watuhumiwa hao wote 6 watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi utakapo kuwa umekamilika na msako huo utakuwa ni endelevu kwa muda wote katika maeneo ya Mkoa huu.
Alieleza jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua za kisheria kwani madhara ya pombe hizo za viroba ni pamoja na uchafuzi wa mazingira ,ongezeko la matumizi ya pombe kali kwa watoto wa shule kutokana na wapesi wa gharama .
MWISHO
No comments:
Post a Comment