Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu Athumani Issa Mkazi wa Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kuiba Ng-ombe aliyekuwa na mimba MTAMBA na kisha kumchinja na nyama yake kuiuza kwenye Bucha yake.
.Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Odilo Amwol baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotplewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka .
Awali mwendesha mashitaka mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Michael Peter alidai Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo hapo Novemba 26 mwaka jana huko katika Kijiji cha Shankala Wilayani Mpanda .
Alidai kuwa siku hiyo ya tukio mshitakiwa Athumani Issa aliiba Ng-ombe jike mwenye mimba Mtamba aliyekuwa amezaliwa na Ng-ombe anaeitwa Posta mali ya Said Abdalla Mkazi wa Kijiji cha Shankala
Mwanasheria huyo wa Serikali aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa baada ya kuwa ameiba Ng-ombe hiyo aliichukua hadi nyumbani kwake katika mtaa wa Kawajense na kuichinja usiku huo huo na kisha asubuhi alikwenda kuuza nyama kwenye bucha yake .
Kabla ya kusoma hukumu Hakimu Mkazi Amwol alimtaka mshitakiwa kama atakuwa na sababu yoyote ya msingi ya kuishawishi Mahakama impunguzie adhabu aeleze mbele ya Mahakama .
Katika utetezi wake mshitakiwa aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana watoto wake ambao anawalea waliofiwa na mama yao na pia mama yake mzazi anamtegemea yeye .
Baada ya utetezi ho mwanasheria wa Serikari Michael Peter aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa huyo hana rekodi nyingine ya inayomuanyesha kuwa aliwahi kushitakiwa tena .
Hakimu Amwol alisoma hukumu kwa kuieleza Mahakama kuwa Mahakama imempa adhabu mshitakiwa Athumani Issa ya kifungo cha miaka saba jela na pia akitoka alipe fidia ya kiasi cha Tshs 550,000 mwa mwenye Ng-ombe.
MWISHO
No comments:
Post a Comment