Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Wachimbaji wa dogo wa madini wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutumia vizuri ruzuku wanayopewa na Serikali ili iweze kutumika kama ilivyokusudiwa na ilete tija kwa sekta ya wachimbaji wadogo hapa Chini.
Mafunzo hayo ya siku moja yaliondaliwa na Wizara ya Nishati na Madini yaliowashirikisha wanaufaika wa ruzuku ya wachimbaji wadogo wa madini na wachimbaji wadogo yalifunguliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga katika ukumbi wa idara ya maji mjini hapa.
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo Muhuga alisema Serikali inatambua umuhimu wa michango inayotokana na wachimbaji wadogo wa madini katika kuinua uchumi wa wachimbaji wenyewe na pato la Taifa kwa ujumla .
Alisema swala la ujasiriamali katika shuhuli za madini ni muhimu kwa maendeleo ya jamii ya uchimbaji mdogo umefaka wakati sasa wa kuendelea kuifanya sekta hii ya uchimbaji mdogo wa madini kuwa ya heshima zaidi tafauti na miaka ya nyuma ambapo uchimbaji mdogo wa madini walionekana kama watu waliokata tama.
Lakini sasa kupitia sekta hii mafanikio yameanza kuonekana kwani baadhi ya wachimbaji wadogo baada ya kuuza madini yao wameweza kuwekeza kwenye miradi mingine isiyo hamishika.
Alisema Serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta ndogo ya uchimbaji wa madini itaendelea na juhudi zake za kutoa msaada wa kila aina hii kuwezesha na kuboresha uchimbaji mdogo na biashara ya madini nchini .
Hivyo aliwaasa wachimbaji wote wadogo popote walipo Tanzania kwamba pale Serikali inapowateuwa kuwapatia mafunzo basi wawe tayari kushiriki kikamilifu ili mafunzo watakayopewa yaweze kuwasaidia serikali katika kupambana na wale wasio na maadali katika uchimbaji na biashara ya madini .
Nae Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na madini Pro James Mdoe alieleza kuwa Serikali inawategemea sana wachimbaji wadogo kwa ajiri ya kuongeza ajira hapa nchini .
Alsema wachimbaji wengi wadogo hapa nchini wameshindwa kuwa wachimbaji wa kati kutokana na kufanya kazi zao bila kuwa na takwimu hivyo aliwashauri wafanye kazi zao kwa kutunza takwimu ambazo zinakuwa sahihi .
Nao washiriki wa mafunzo hayo Said Gecha kutoka Katavi , Grece Mgina Iringa na Hassan Doyo walisema watu wengi walikuwa hawaamini kama serikali inaweza kutowa ruzuku kwa wachimbaji wadogo lakini sasa wameamini kilichofanywa na serikali ambapo ruzuku iliyotolewa itasidia kuinua uchumi wa wachimbaji mmo ja mmoja na taifa kwa ujumla.
Mafunzo hayo yaliwashirikisha pia wachimbaji wadogo wa madini wa kutoka Mikoa yote hapa nchini na wanafaika 59 waliopatiwa ruzuku ya awamu ya tatu na makamishina wasaidizi kutoka Kanda zote za hapa Tanzania .
MWISHO
No comments:
Post a Comment