Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Wachimbaji wa madini wametakiwa kufanya shughuli zao kwa kujipusha na uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na shughuli za uchimbaji katika maeneo ya migodi iwapo taratibu za hifadhi hawatazizingatia kikamilifu .
Hayo yalisemwa hapo jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja ya wanufaika wa ruzuku ya wachimbaji wadogo wa madini yaliowashirikisha wachimbaji wadogo na wanufaika wa ruzuku wa kutoka Kanda zote za hapa nchini . yalifanyika jana katika ukumbi wa maji mjini Mpanda.
Alisema lipo jambo ambalo ni dhahiri kabisa lipo katika mchakato wa uchimbaji wa madini ambalo ni uharibifu wa mazingira unaosababishwa na shughuli za uchimbaji katika maeneo ya migodi unao tokana na wachimbaji kutozingatia taratibu za hifadhi ya mazingira kikamilifu .
Ili kuleta maendeleo ya kweli katika shughuli ya madini aliwasihi wachimbaji wazingatie utunzaji wa mazingira katika maeneo yao ya kazi .
Aidha aliwataka wawakemee wale wote wanaochoma misitu kwa kisingizio cha kutafuta madini hasa ya vito na dhahabu na pia haitakuwa jambo la busara kuchafua vyanzo vya maji , kutupa ovyo mabaki yanayotokana na uchimbaji
Alisema. Serikali itaendelea kutenga kutenga fedha kiasi cha fedha kwa ajiri ya ruzuku kitakachotumika kununulia vifaa vya uchimbaji .
Muhuga alieleza kuwa nia ya Serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini kuendeleza shughuli zao za uchimbaji wa madini na itaendelea kutenga kiasi cha fedha kwa ajiri ya ruzuku kitakacho tumika kununulia vifaa vya uchimbaji .
Alifafanua kuwa ni azima ya Serikali kendelea kufanyia kazi cha ngamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya madini hapa nchini .
Kwa upande wake Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Pro James Mdoe alisema kwa upande wa Serikali ari ya kuunga mkono juhudi za wachimbaji wadogo imeonekana katika mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na .
Kutowa ruzuku inayowezesha kupatikana kwa vifaa vya kisasa vya uchimbaji na uchenjuaji madini, kuboresha na kurahisisha utoaji wa leseni ndogo za madini ambapo sasa zinapatikana mikoani badala ya Dares salaam.
MWISHO
No comments:
Post a Comment