Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho wa Mkoa wa Katavi Mselemu Abdala pamoja na Wandishi wa Habari watatu wamenusurika kifa baada ya gari lao walilokuwa wakisafiria kupata ajari kwa kugonga gema la utuka wa barabara na gari kugonga mti na kuingia kichakani wakati wakitokea kwenye uzinduzi wa kampeni za kugombea udiwani wa Kata ya Kasansa Tarafa ya Mamba Wilayani Mlele .
Ajari hiyo ilitokea hapo juzi majira ya saa tatu na nusu ya usiku katika eneo la sikiiko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi barabara ya kutoka Mpanda kuelekea Mipmwe Wilayani Tanganyika
Ajari hiyo ililihusisha gari lenye Namba za usajiiri T 604 TEU aina ya Toyota Land Crusa. Mali ya CCM Wilaya ya Mpanda lililokuwa likiendeshwa na Chares Emanueli 54 Mkazi wa Mtaa wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda .
Viongozi hao wa CCM wa Mkoa wa Katavi na Wandishi wa Habari watatu walikuwa wakitokea kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa kugombea Udiwani wa Kata ya Kasansa ulizinduliwa juzi uliopangwa kufanyika Januari 22 kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo Sisto Cherehani CCM na unavishirikisha vyama vya Chadema na Ccm.
Viongozi hao walionusurika kifo katika ajari hiyo ni Mwenyekiti wa Ccm wa Mkoa wa Katavi Mselemu Abdalla , Katibu Mwezi wa Mkoa Joseph Makumbule Kaimu Katibu wa Mkoa ambae pia ni katibu wa Wilaya ya Mpanda, Katibu wa Wazazi, Katibu wa Uwt wa Wilaya ya Mlele Kaimu kativu wa uvc wa Mkoa ,mjumbe wa kamati ya siasa wa Mkoa Jeneroza Mmbamba na Wandishi w Eneresti Kibada wa Azamu TV Mwandishi wa gazeti Mtanzania Walter Mguluchuma na Mtangazji wa Radio Pamoja Fm Edwin Sangu .
Kabla ya ajari hiyo gari hilo lilikatika siteligi rood na kisha liligonga gema la barabara kwa upande wa kushoto na kisha lilibadili mwelekeo na kuelekea upande wa pili wa barabara na kuacha njia kugonga mti na kuingia vichani .
Katika ajari hiyo watu wote walilazimikaa kukaa ndani ya gari hilo kwa zaidi ya dakika kumi huku wakiwa hawaamini kile ambacho kilikuwa kimetokea na hakukuwa na mtu ambae alikuwa amejeruhiwa katika ajari hiyo .
Viongozi hao na wandishi wa Habari walikuja kapatiwa msaada kutoka kwa askari wa Hifadhi Katavi baada ya kuwa wamekaa kwenye eneo hilo kwa muda wa saa saa mbili .
MWISHO
No comments:
Post a Comment