Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi kimezindua kampeni i za uchaguzi mdogo wa kugombea udiwani katika Kata ya Kasansa Tarafa ya Mamba Wilayani Mlele Mkoani Hapa .
Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Kijiji cha Igalukilo kampeni za chama hicho zilizinduliwa na Mwenyekiti wa ccm wa Mkoa wa Katavi Mselemu Abdala na unavishirikisha vyama vya ccm na Chadema .
Uchaguzi huo mdogo wa udiwani ulipangwa kufanyika January 22 utafanyika ufatia kifo cha aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo Sisto Charahani ccm aliyefariki Dunia Oktoba mwaka jana na imemteuwa Silasi Ilumba kuwa ndiye mgombea wao kwenye uchaguzi huo .
Akizindua Kampeni hizo Mwenyekiti wa ccm Mselemu Abdala alisema endapo mwanachama yoyote wa chama hicho atakae bainika kukisaliti chama hicho kwenye uchaguzchama hakitasita kumchukulia hatua .
Alisema itakuwa ni jambo la kushangaza kwa ccm kushindwa kupata ushindi kwenye Kata hiyo kwa kuwa wao ni wengi kuliko Chadema hivyo endapo watashindwa lazima watatazamana ili kumjua mtu aliyekisaliti chama .
Aliwataka wananchi wa Kata hiyo kuacha tabia ya kubaguana kutokana na maeneo ya Vijijini wanayokuwa wanatoka wagombea na wala wasiingize udini na ukabila kwenye maswala ya uchaguzi kwani Watanzania wote ni wamoja .
Mselemu alisema wakati wa kura za maoni ndani ya chama hicho za kumpata mgombea wao wa udiwani kulikuwa na ubaguzi wa maeneo ambayo walikuwa wakitoka wagombea ndani ya chama hicho hivyo ni budi sasa waugane na wasiendelee kufanya hivyo kwani sio jambo jema .
Alionya watu wa Kata hiyo wasifanye utani kwenye maswala ya dini kwenye uchaguzi na wasichanganye matatizo yao na siasa na pia wasilte mambo ya mzaa kwenye mambo ya maendeleo .
Alisema ccm wamejiwekea utaratibu mzuri wa kuwapata wagombea wao wa nafasi mbalimbali na ndio maana wamekuwa wakishinda kutoka na utaratibu wao huo walijiwekea wa kuwapa wagombea wao .
Watu ambae wamukuwa wakikimbilia kugombea nafasi za uongozi wanapaswa kutambua unawezaa kuchaguliwa vizuri lakini utatoka vibaya .
Katika uzinduzi huo jumla ya wanachama sabini kutoka vijiji vinne vya Kata hiyo walirudisha kadi za Chadema na kujiunga na Ccm.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mlele Leacho Kasanda ambae pia Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya Wilaya hiyo alivitaka vyama ambavyo vinashiriki uchaguzi huo kufuata sheria za nchi .
Alisema vyama vyote lazima vitambue kuwa vipo shini ya sheria hivyo kwenye kipindi hiki cha uchaguzi wafanye kampeni zao kwa kuata sheria za nchi na serikali ya Wilaya ya Mlele ipo tayari kuvilinda vyama vyote bila ubaguzi wowote .
Alisema watahakikisha uchaguzi huo mdogo unafanyika kwa amani katika kipindi chote cha uchaguzi kwao wamejipanga kuhakikisha hakutokei uvunjwaji wa amani kwenye uchaguzi huo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment