.
Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Baadhi ya Wakazi wa Mkoa wa Katavi wameanza kulazimika kura mlo mmoja wa chakula kutokana na kupanda mara dufu kwa bei ya zao la mahindi na unga wa sebe katika Wilaya zote za Mkoa wa Katavi .
Mmoja wa Wakazi wa Kijiji cha Igagala Wilaya ya Mpanda Onesmo Maweli alieleza kuwa kwa sasa analazmika kula mlo mmoja wa chakula kutokana na kupanda mara dufu kwa bei ya mahindi na unga wa sebe tofauti na mwaka uliopita .
Alifafanua kuwa debe moja la mahindi lenye ujazo wa kilo 18 wananunua kwa bei ya Tsh 16,000 na wanakoboresha kwa shilingi elfu moja na kusaga kwa shilingi elfu moja hivyo hadi uweze kupata unga kwenye debe moja la mahindi unalazimika kutumia Tsh 18,000. Mwaka jana mwezi kama huu walikuwa wakinunua debe moja kwa Tsh 8,000
Alisema kutokana na kupanda huko kwa bei ya mahindi wakazi wengi wa Vijijini ambao chakula chao kikubwa ni ugali wanalazimika kula mlo mmoja tuu wa chakula .
Wanachokifanya kwa sasa badala ya kula mapema wanalazimika kula chakula kwa muda wa kuchewa ili waweze kula mmlo mmoja tuu kutoka na hari ya uchumi mdogo walionao alisema Mawela .
Alieleza kuwa wanao kuwa wanaathirika zaidi na kula mlo mmoja kwenye maeneo ya vijijini ni wale watu ambao wanafamilia ya watu wengi kama yeye .
Nae Abel Kalifumu Mkazi wa Kijiji cha Uzega Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele alilalamikia kupanda ghafla kwa bei ya unga wa sembe kwa kipindi kifupi tuu cha mwezi mmoja katika katika Tarafa ya Inyonga ambayo ndio makao makuu ya Wilaya ya Mlele .
Alisema bei ya unga wa sebe yenye uzito wa kilo 25 iliyokuwa ikiuzwa kwa bei ya tsh 26,000 mwezi uliopita sasa hivi inauzwa kwa bei ya Tsh 32,000 na debe la mahindi linauzwa kwa bei ya Tsh 15,000 hari ambayo inawafanya watu waanze kula mlo mmoja kwa siku .
Kalifumu alieleza kuwa wameingiwa na mashaka ya kuwepo kwa dalili za kupanda kwa bei ya mahindi ifikiapo mwezi January kwani mwaka jana mwezi kama huu waliuwa wakinunua debe moja la mahindi kwa bei ya Tsh 7,000
Hivyo aliiomba serikali ya Mkoa wa Katavi kuona uwezekano wa kusambaza mahindi yalioko kwenye maghara ya Hifadhi ya akiba ya chakula yalioko Mpanda na kuwauzia wananchi kwa bei nafuu .
MWISHO
No comments:
Post a Comment