Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa ni Katavi Imemuhukumu Ndeisaba Masud 35 Mkazi wa Makazi ya Wakimbi ya Katumba Wilaya ya Mpanda kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na meno ya Tembo vipande 25 yenye thamani ya shilingi Milioni 148.
Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka .
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka Mwanasheria w a Serikali wa Mkoa wa Katavi Jamira Mziray aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo hapo January 12 mwaka 2015 huko katika Kijiji cha Urwila Wilaya ya Mpanda .
Siku HIyo ya tukio mshitakiwa Ndeisaba a likamatwa na meno hayo ya Tembo akiwa ameyapakia kwenye begi mbili ndani ya basi la Kampuni ya AM lililokuwa likifanya safari kutoka Mpanda kuelekea Mkoani Tabora .
Mwendesha mashitaki Mziray aleleza kuwa kabla ya kukamatwa kwa mshitakiwa Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na jeshi la polisi walikuwa wamepata taarifa kutoka kwa Raia wema juu ya mshitakiwa kuwa anamipango ya kusafirisha meno ya Tembo kutoka Katumba na kuyapeleka Mkoani Tabora kwa kutumia basi la Kampuni ya AM.
Alidai kuwa baada ya kuwa wamepata taarifa hizo Askari wa Hifadhi ya Katavi na Polisi walianda mtego na ndipo waliweza kufanikiwa kumkamata mshitakiw akiwa ndani ya basi hil na walipompekua kwenye mizigo ya beji zake mbili alizokuwa amepakia kwenye basi la Kampuni ya AM waliweza kumkamata na meno ya Tembo vipande 25 vyenye thamani ya Tsh Milioni 148 mali Serikari ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania .
Hakimu Chiganga kabla ya kusoma hukumu hiyo alieleza kuwa kutokana ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka Mahakama pasipo shaka yoyote imemwona mshitakiwa amepatikana na hatia ya kifungo cha sheria Namba 235 cha kanuni ya adhabu na sheria ya wanyama pori ya mwaka 2009.
Kutoka na kupatikana hatiia hiyo Hakimu Chiganga alimtaka mshitakiwa kama anayosababu yoyote ya msingi ya kuishawishi Mahakama impunguzie adhabu basi mahakama ilitowa nafasi kwa mshitakiwa kuweza kujitetea kabla ya kusomewa hukumu .
Katika utetezi wake mshitakiwa aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kile achodai kuwa bado umri wake ni mdogo na pia ameowa hivi karibuni hata hivyo maombi hayo yalipingwa vikali na mwendesha mashitaka mwanasheria wa Serikali ambae aliiomba Mahakama itowe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwefundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo .
Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga Ntengwa akisoma hukumu hiyo aliambia Mahakama kuwa Mahakama imemuhukumu mshitakiwa Ndeisaba kifungo cha miaka 20 kuanzia jana baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na meno ya Tembo vipande 25 vyenye thamani ya milioni 148 mali ya Serikali ya Jmhuri ya Muungano wa Tanzania na aliamuru meno hayo ya Tembo yakabidhiwe Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa ajiri ya kuyahifadhi .
Katika kesi hiyo Mahakama hiyo ilimwachia huru mshitakiwa wa pili aitwaye Samson Fedrick Mkazi wa Makazi ya Wakimbi ya Katumba baada ya upande wa mashitaka kushindwa kutowa ushahidi wa kumtia hatia mshitakiwa .
No comments:
Post a Comment