Na Walter Mguluchuma Katavi.
WazirI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa anatarajiwa kuanza kufanya ziara ya siku nne Mkoani Katavi ambapo atatembelea na kukagua miradi mbalimbli ya maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi kwenye Mikutano ya hadhara itakayofanyika katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi .
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Katavi Lautel Kanoni ziara hiyo ya Waziri Mkuu Majaliwa inatarajiwa kuanza leo Agosti 20 hadi Agosti 23 .
Kwa mujibu wa ratiba hiyo Waziri Mkuu atawasili katika uwanja wa Ndege wa Mpanda leo mchana kwa ndege na kisha ataelekea Ikulu Ndogo ya Mpanda ambapo atasomewa taarifa ya Mkoa na kisha atazungumza na watumishi wa Serikali katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Mpanda.
Siku itakayofuata atakwenda katika Kijiji cha Majalila kwa ajili ya kuona eneo zitakapojengwa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na kutembelea mradi wa maji katika Kijiji hicho na kisha atawahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara.
Siku hiyo pia atawahutubia Wananchi katika mikutano ya hadhara itakayofanyika katika eneo la Kijiji cha Ndui Makazi ya wakimbizi ya Katumba na katika uwanja wa Azimio Mjini Mpanda .
Agsti 22 Waziri Mkuu atafanya ziara ya siku moja katika Wilaya ya Mlele ambapo atawahutubia wananchi wa Inyonga katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na na baadaye elekea katika Kijiji cha Majimoto Halmashari ya Mpimbwe na atakagua ujenzi wa Daraja la mto Kavuu na kisha atawahutubia wananchi wa Kijiji hicho katika mkutano wa Hadhara.
Waziri Mkuu Majaliwa Agosti 23 atafanya mkutano wa majumuisho ya ziara yake katika ukumbi wa Idara ya Maji Mjini hapa na ataelekea Wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa .
Baada ya ziara yake Mkoani Rukwa Majaliwa siku ya tarehe 26 atakwenda Kijijini kwake Mizengo Kijiji cha Kibaoni Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi ambapo atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda na kasha atatembelea shule ya Msingi ya Kakuni aliyosoma Pinda na siku hiyo hiyo ataondoka kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda ikiwa ndio mwisho wa ziara yake ya mikoa ya Katavi na Rukwa .
No comments:
Post a Comment