Walter Mguluchuma
Katavi
Wakulima wa vyama vya ushirika wa Tumbaku katika Mkoa wa Katavi wanatarajia kuzalisha na kuuza zaidi ya kilo Milioni 9.2 za Tumbaku katika msimu wa kilimo wa 2015 na 2016 uzalishaji huo ukiwa umeshuka kiwango cha asilimia 22 ya uzalishaji wa msimu uliopita wa 2014 na 2015 ambapo zilizalishwa na kuuzwa kilo Milioni 11.9.
Hayo yalisemwa hapo juzi katika risala ya Wakulima wa Tumbaku wa Mkoa wa Katavi iliyosomwa na Mwenyekiti wa Chama kikuu cha ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Mkoa wa Katavi LATCU Modesti Yamlinga mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenelali Mstaafu Raphael Muhuga wakati wa sherehe za uzinduzi wa masoko ya ununuzi wa Tumbaku wa msimu wa 2015 na 2016 zilizofanyika katika Kijiji cha Igagala chama cha Msingi Mpandakati .
Yamlinga alisema katika msimu huu wa 2015 na 2016 Wakulima wa vyama vya ushirika wa Tumbaku wanatarajia kuzalisha na kuuza Tumbaku yenye jumla ya Kilo 9,265,796 ukiwa umeshuka kwa asilia 22.21 ukilinganisha na uzalishaji wa msimu wa kilimo uliopita wa 2014 na 2015 ambapo uzalishaji wa Tumbaku ulikuwa ni kilo 11,910,459.
Alieleza kuwa bei ya Tumbaku huwa inapangwa mapema na Tobacco Council kabla ya msimu hauja anza hivyo mkulima huwa anakuwa na uhakika na bei ya kuuzia zao lao mapema .
Katika sekta ya Tumbaku wamejiwekea utaratibu wa kufuata kanuni za kilimo cha Tumbaku kwa kila mkulima kupanda miti na kila Chama cha ushirika cha msingi kinatakiwa kiwe na shamba la miti ikiwa ni pamoja na kutunza miti ya asili.
Mwenyekiti huyo wa Latcu alisema katika vipindi hivyo viwili vya msimu wa 2014 hadi 2016 Wakulima wa vyama vya msingi vya ushirika wa Wakulima wa Tumbaku wameweza kupanda hadi sasa miche ya miti 8,919,206.
Alivitaja vyama vya Msingi saba vya Wakulima wakulima wa Tumbaku vilivyoko katika Mkoa wa Katavi kuwa ni Ilunde,Ukonongo,Katumba , Nsimbo , Mpandakati , Kasokola na Mishamo na Makampuni yanayonunua Tumbaku Mkoani hapa ni TLTC na Premium.
Baadhi ya changamoto zinazo wakabili wakulima wa Tumbaku alizitaja kuwa ni ubovu wa barabara katika maeneo yanayozalisha Tumbu na wakulima kutokuwa waaminifu kwa kuwauzia watu tumbaku yao ambao sio wakulima hari ambayo imefanya baadhi ya wakulima kushindwa kulipa madeni yao .
Changamoto nyingine ni uchomaji holela wa moto kwenye mashamba ya miti unaofanywa na raia wengine pamoja na uchache wa Makampuni yanayonunua Tumbaku hari inayosababisha kutokuwepo kwa ushindani wa biashara.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliwataka viongozi wa vyama vya Msingi wasimamie majukumu yao kikamilifu ili wakulima wao waweze kupata malipo sitahiki.
Alisema wapo viongozi na wanachama wanao saliti ushirika ni vizuri mkawashughulikia haraka kwa mujibu wa sheria ili kuunusuru ushirika wa zao la Tumbaku kwa ujumla wake .
Meja jenelali Muhuga aliwataka viongozi wa vyama vya Msingi kuhakikisha wanaandaa orodha sahihi ya wanachama na wasio wanachama ,kwani wanaosadikiwa kuleta vurugu kwenye vyama vya msingi vya ushirika wengi wao si wanachama wa vyama vyao na hao ndio wanauwezo wa kuweka maazimio mabovu .
Tekelezeni hilo na nipate taarifa kabla ya masoko ya Tumbaku ya msimu huu niliyofungua hajafikia mwisho alisema Meja Jenelali Mstaafu Raphael Muhuga .
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima alisema zao la Tumbku ndio zao mama katika Mkoa wa Katavi ambalo linamwingizia pesa mkulima kuliko mazao mengine .
Hivyo wanaushirika wa Tumbaku wasikubali kuuwa ushirika wao kwani ndio umekuwa mkombozi wa kuwasaidia watu wa kipato cha chini .
No comments:
Post a Comment