Na Walter Mguluchuma
Katavi
Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi wengi wao wakiwa ni Wanafunzi wa kiume katika Shule za Msingi na Sekondari wako katika hatari kubwa ya kupata magonjwa mbalimbali yatokayo na Ngono ukiwemo Ukimwi baada ya kushamiri kwa biashara ya kuuza miili kufutia kundi kubwa la madada poa kuvamia Mji wa Mpanda na kukodi nyumba mbili za kulala wageni na kisha kufanya biashara ya kujiuza kwa bei ya kuanzia shilingi 2000 huku wateja wao wakubwa wakiwa ni wanafunzi wa Sekondari na shule za Msingi.
Biashara hiyo ya ngano imeshamiri zaidi katika Mtaa wa Majengo B ambao unajulikana kwa jina la maarufu kuwa ni Mtaa wa FISI baada ya akina Dada poa kuhama katika mikoa mingine na kuhamia Wilayani Mpanda huku wengi wao wakiwa wanatoka katika Mikoa ya Mwanza, Mbeya na Kigoma.
Dada poa hao ambao wamegundua mbinu mpya badala ya kukaa kwenye madanguro wao wameamua kukodi nyumba mbili za kulala wageni ambazo zipo jirani jirani katika Mtaa huo ambazo majina zake tuunayo kwa ajiri ya kufanya biashara hiyo ya Ngano .
Gazeti hili lilizungukia juzi kwenye eneo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa mtaa huo lilishuhudia makundi makubwa ya vijana wakiwa wamepanga foleni kwa ajiri kuingia ndani ya nyumba hizo za kulala wageni huku baadhi ya akina dada poa hao wakiwa wanalandalanda na wamevaa nguo zisizo za heshima.
Akizungumza na gazeti hili mmiliki mmoja wa Bar inayouza vinywaji vikari alisema biashara hiyo imekuwa ikifanyika zaidi kuanzia saa moja ya usiku hadi saa sita usiku .
Mmoja wa dada poa hao akizungumza na gazeti hili akiwa kwenye bar ya Zebra ilipo kwenye mtaa huo ambae yeye alijitambulisha kuwa ni mkazi wa kutoka Mkoa wa Mwanza alisema yeye na wenzake waliamua kuacha kuishi kwenye nyumba za danguro baada ya kuona wa wakikamatwa mara kwa mara wakati wa misako ya polisi .
Alisema toka walipoamua kukodi nyumba hizo mbili za kulala wageni wameacha kusumbuliwa na misako ya mara kwa mara na wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa uhuru tofauti na wakati walipo kuwa wanaishi kwenye madanguro.
Alieleza kutokana na biashara hiyo ya ngono wamekuwa ni sehemu ya watu wanao changia kodi ya Serikali
kwani fedha wanazomlipa mwenye nyumba ya kulala wageni nae analipia kodi ya Serikalini tofauti na tulivyokuwa tukiishi kwenye madanguro hatukuwa tunachangia kodi ya seriakali.
Alifafanua kuwa biashara hiyo wamekuwa wakiifanya kwa viwango tofauti ambapo kima cha chini wamekua wakianzia shilingi 1000 na kina cha juu kikekuwa akizidi shilingi 10,000 ingawa wateja wao wengi ni wale wa kati ya shilingi elfu mbili na elfu
Mkazi wa Mtaa huo Osca Seleman alieleza kuwa wamekuwa wakipata kero kubwa toka wakinada poa hao walipohamia kwenye nyumba hizo za kulala wageni kutokana na kuzagaa kwa makundi ya vijana.
Pia hata vibaka wamekuwa wakizungukia sana kwenye maeneo hayo hari ambayo imekuwa ikiwafanya walale kwa hofu ya kuogapa kuibiwa mari zao hasa simu za mikononi.
No comments:
Post a Comment