Monday, February 22, 2016

TAKUKURU YAMFIKISHA KIZIMBANI ASKARI POLISI KWA TUHUMA ZA KUMKAMATA NA RUSHWA YA TSH 100,000

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
 Katavi
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU  Mkoa wa Katavi imemfikisha mahakamani askari wa jeshi la polisi  wa kituo cha polisi cha Mwese Wilayani Mpanda Peter Kashuta  G,451PC  ambae alishawishi  kuomba rushwa ya Tsh 700,000 ili aweze kumwachia huru mshitakiwa.
Mtuhumiwa huyo alifikishwa jana kimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda na kusomewa mashitaka na  mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Bahati  Haule  mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa.
Mwendesha mashita huyo alidai mahakamani hapo kuwa  TAKUKURU  Mkoa wa Katavi walipata taarifa  kutoka kwa  Ruchege Mambalo  aliyewekwa mahabusu  katika kituo cha polisi Mwese  kwa tuhuma za kumpiga motto wake  aitwaye  Lutobhisha  Mambalo  mwenye matatizo ya akili alipotaka  kumchoma kisu baba yake katika harakati za kujiokoa  alichukua jiwe na  kumpiga nalo usoni.
Baada ya kupigwa na   jiwe  hilo  alikimbia  na kwenda kutoa taarifa  kituo cha polisi Mwese  ndipo  Ruchega Mambalo alimfuata  mtoto wake kituo cha polisi  na alimkuta kituoni hapo akiwa  na Askari Polisi  Peter Kashuta  ambae  alimshawishi na kumwomba Rushwa ya  Tsh 700,000  iliaweze kumwachia huru.
Mwendesha mashitaka huyo wa Takukuru alidai kuwa  baada ya kupokea taarifa hizo za Askari kuomba rushwa  na walianza kufanya uchunguzi wa kina  ili kuweza  kuthibitisha  tuhuma hiyo na ilithibitika   na ndipo mtego  wa Rushwa uliandaliwa .
Aliiambia Mahakama  baada ya mtego kuandaliwa  hatimae Takukuru  walifanikiwa  kumkamata Askari wa Jeshi la polisi Peter Kashuta  akipokea rushwa ya  Tsh 100,000  kutoka kwa  Ruchege  Mambalo  ilikumfutia  tuhuma  ya kumjeruhi mtoto wake.
Hahati Haule aliiambia Mahakama kuwa  tukio la kukamatwa kwa  mtuhumiwa lilitokea Februari  10 huko katika  Kijiji cha Lwega  kata ya  Mwese kwenye mgawaha .
Mshitakiwa alisomewa mashitaka mawili  na mwendesha mashitaka huyo wa Takukuru  Bahati Haule  shitaka la kwanza  kuomba na kushawishi  rushwa ya Tsh 700,000 na shitaka la pili kupokea rushwa ya Tsh 100,000  kinyume  na matakwa ya mwajiri wake  kwa mijibu  wa kifungu cha sheria  15 kidogo cha kwanza (a( cha sheria  ya kuzuia na kupambana na rushwa  namba 7 yamwaka 2007.
Baada ya kusomewa mashitaka mtuhumiwa alikana mashitaka hayo  na Hakimu mkazi Chiganga Ntengwa alimwachia  kwa dhamana  baada ya kukidhi  mashaliti ya dhamana  ambayo ni  kuwa na mdhamini  mmoja mwenye  hati ya nyumba  au fedha tasilimu  shilingi milioni mbili  na kutosafiri nje ya Mkoa wa Katavi  bila kibali  cha mahakama  ya Wilaya ya Mpanda.

No comments:

Post a Comment