Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Askofu wa Kanisa Katoloki Jimbo la Mpanda Gervansi Nyaisonga amewataka madiwani wa Manispaa ya Mpanda wasaidie kuwaelimisha watu juu ya waraka wa elmu bure na vipengele muhimu kwenye waraka huo vitafusiliwe kwa lugha nyepesi.
Ushauri huo aliutowa hapo jana ofisini kwake wakati alipokuwa akizungumza na madiwani wa Manispaa ya Mpanda walikwenda kumtembelea na kumwelezea mikakati yao ya mipago ya maendeleo wakiongozwa na meya wa Manispaa hiyo Willy Mbogo.
Askofu Nyaisonga alisema watu waliowengi hawauelewi waraka wa elimu bure hivyo ni wajibu wa madiwani kusaidia kuwaelimisha watu waufahamu vizuri waraka wa elimu bure.
Alieleza pamoja na kutolewa kwa waraka huo upo umuhimu mkubwa ukatafusiliwa kwa lugha nyepesi hasa kwenye vipengele vile vyepesi ili wananchi wauelewe vizuri na yeye yuko tayari kuwaelimisha waumini wake waraka huo .
Alisema madiwani watambue kuwa wao ni watu muhimu kwenye jamii hivyo wathamini majukumu yao wajue wapo kwa ajiri ya watu hivyo wanaowajibu wa kuisimamia Manispaa yao na watu wasiende kwenye siasa ili wakaibe .
Pia aliwataka madiwani hao wahamasishe watu wawekeze katika uwekezaji kwani furusa za uwekezaji zipo nyingi na wajitahidi kukusanya mapato yao ya ndani kuliko kutegemea bajeti ya kutoka Serikalini ambayo haitoshi kuendesha shughuli za maendeleo.
Makamu wa Askofu Padri Patrick Kasoma nchi ilikuwa na changamoto ya watu kuwa wamekaa bila kuwa wanafanya kazi na walikuwa wanajua kura tuu kuliko kufanya kazi .
Mtu anaetaka kuwa kiongozi ajivue kwanza uvivu na ubinafsi ndio aweze kuwaongoza watu na madiwani wajitahidi kusimamia usafi kwani mji utakapokuwa msafi magonjwa ya kuambukiza yatakwisha alisema Padri Kasomo.
Alisema viongozi wengi wamekuwa wakikosa imani kwa wananchi wao kwa kuwa walikuwa hawauziki na walikuwa walikuwa wakichaguliwa kwa ajiri ya fedha .
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Mpanda Wiliy Mbogo alisema wanalengo la kuimarisha Halmashauri yao kwa kuongeza vyanzo vyao vya ukusanyaji wa mapato .
Na swala la madiwani kwenda
kuwatembelea na kupokea maoni na ushauri kutoka kwa viongozi wa
madhehebu ya dini litakuwa ni endelevu katika Manispaa ya Mpanda kwani viongozi hao wa dini wanayo nafasi kwenye jamii.
No comments:
Post a Comment