Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Naibu Waziri wa Kilimo uvuvi na ufugaji Wiliamu Ole Nasha ameuagiza uongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanapima wanaweka mpango
bora wa matumizi ya ardhi kwa kupima ardhi na kuitenga kwa ajiri ya
matumizi mbalimbali ili kuepukana na migogoro ya mara kwa mara ya
Wakulima na wafugaji.
Nasha alitowa agizo hilo hapo jana wakati alipokuwa akiwatubiwa Wananchi wa Kijiji cha Mwamkulu Wilayani Mpanda kwenye mkutano wa hadhara.
Alisema migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji imekuwa ititokea hapa Nchini mara kwa mara kutokana na kutokuwepo kwa mipango bora ya matumizi ya ardhi kwa kuitenga kwa ajiri ya matumizi mbalimbali.
Alieleza Serikali ya awamu ya tano imepanga kuhakikisha inashughulikia na kumaliza migogoro yote ya ardhi ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikiendelea kutokea .
Alifafanua kuwa Serikali inautegemea sana Mkoa wa Katavi kwa ajiri ya uzalishaji wa mazao ya chakula hivyo viongozi wa Mkoa huo waakikishe wanaweka mipango boraya matumizi ya adrhi kabla ya haija haijaalibiwa kwani uongozi wa Mkoa huo wanayonafasi ya kufanya hivyo,
Nasha alisema Mkoa wa Katavi ni Mkoa ambao unapokea watu wengi wanao toka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wanao hamia hapo kwa ajiri ya kufanya shughuli za ufugaji na kilimo hivyo wasipokuwa na mipango mizuri ya matumizi bora ya ardhi upo uwezekano mkubwa wa kuharibika kwa ardhi ,
Pia ameutaka uongozi wa Serikali kuhakikisha watu wanao hamia Mkoani hapo hawahamii kiholela bali wahamie kwa kufuata utaratibu wa sheria .
Naibu Waziri Nasha vilevile amewataka watendaji wa Serikali kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa kwani Serikali imepanga kuwa karibu na wananchi kwa kusikiliza na kushughulikia na kutatua kero za wananchi hivyo watendaji waache kukaa ofisini bali waende kusikiliza kero za wananchi.
Alisema Serikali imejipanga kuhakikisha pembejeo za kilimo zinamfikia mkulima kwa wakati na inamchulia hatua mtu yoyoye ambae atasababisha pembejeo zishindwe kufika kwa wakati kwa mkulima .
Nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Madeni Kipande alimwakikishia Naibu Waziri kuwa Mkoa huo utaanza kutekeleza agizo la upimaji wa ardhi kwa ajiri ya mipango bora ya matumizi bora ya ardhi kwa kutumia fedha zao za makusanyo ya ndani bila kusubilia fedha za kutoka Serikali kuu kwani jambo hilo walalichukulia kwa umuhimu mkubwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima alieleza kuwa watu wamekuwa wakihamia Mkoani Katavi kutokana na Mkoa huo kuwa na ardhi kubwa .
Alisema Mkoa huo ndio Mkoa pekee kwa sasa ambao ardhi yake ni yenye rutuba nzuri na ambayo haija alibiwa .
Naibu
Waziri Nasha amemaliza ziara yake ya siku tatu ambayo ilikuwa na lengo
la kuhamasisha maendeleo na kushughulikia malalamiko ya wakulima wa
Tumbaku wa vyama vya ushirika wa Tumbaku vya Mpanda Kati na Ukonongo .
No comments:
Post a Comment