Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari.
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linamshikilia mkazi wa
mji wa Mpanda, kwa tuhuma za kumnyanyasa kwa kumnyima mahitaji muhimu
mtoto wake ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa juzi, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema polisi walipata
taarifa hiyo kupitia kituo kimoja cha radio kilichopo mkoani humo wakati
mtoto huyo akihojiwa.
Alisema baada ya polisi kusikia kipindi hicho, walifuatilia na
kumpata mtoto huyo na kumhoji na kubaini kuwa mzazi wake amekuwa
akimnyima mahitaji muhimu ya kimaisha kama mavazi, chakula, matibabu na
mahitaji ya shule.
Kamanda Kadavashari alisema mtoto huyo tangu mama yake mzazi
afariki dunia mwaka jana na baba yake kuoa mke mwingine, maisha yake
yalibadilika na kuanza kuishi maisha ya manyanyaso na mateso, hali
iliyomsababisha hata kushindwa kuendelea vizuri na masomo.
Alisema katika kanisa ambalo mzazi huyo anasali pamoja na mtoto
huyo, imekuwa ikitolewa michango kwa lengo la kumsaidia lakini mtoto
huyo hamfikii na kwamba hivi karibuni baba yake alimfukuza nyumbani na
kuanza kuishi kwa kutangatanga mitaani.
Kamanda huyo wa polisi mkoa wa Katavi, alisema baada ya baba wa
mtoto huyo kusikia kipindi hicho cha radio, alikwenda polisi kutoa
taarifa za kupotelewa na mtoto wake huyo na polisi kumshikilia na
walipomuhoji walibaini amekuwa akimnyanyasa mtoto wake na tayari
amefunguliwa mashtaka na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili.
CHANZO:
NIPASH.
No comments:
Post a Comment