Wednesday, December 16, 2015

ZAIDI YA EKARI 1200 ZA MAENEO TENGEFU ZAHARIBIWA MPANDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
Zaidi ya Ekari 1,200 za ardhi za maeneo tengefu  zimeharibiwa Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kutokana  na watu  kufanyia  shughuli za kibinadamu na ufugaji wa mifugo
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza  Mwamlima  alieleza hayo hapo jana  mbele ya waandishi wa habari  ofisini kwake  wakati alipokuwa akitowa taarifa za  shughuli  zilizo tekelezwa na Serikali ya Wilaya ya Mpanda kwa kipindi cha mwezi mmoja
Alisema  jumla ya ekari  1,240 za maeneo  tengefu ya ardhi   zimaharibiwa  Wilaya Mpanda  kutokana na watu kuvamia maeneo hayo  na kufanya  shughuli za kibinadamu
 Alitaja sababu ya maeneo  hayo kuharibiwa  kuwa ni watu kufanya  shughuli  za kilimo  kujenga makazi ya kuishi na kufanyia shughuli za ufugaji wa mifugo ya aina mbambali
 Alisema  kutokana na uharibifu huo Wilaya imejipanga kuhakikisha  maeneo hayo yaliharibiwa yanarudia katika hari yake ya kawaida  na pia maeneo mengine  yasiharibiwe
Alifafanua kuwa  kutokana na hari hiyo ya uharibifu wa maeneo tengefu ya ardhi  wameanza kuchukua hatua mbalimbali  za kukabiliana na tatizo hilo
 Mwamlima alizitaja hatua walizochukua ni  kuwaondoa  wavamizi  waliovamia  misitu  na  wamewakamata na wamewafikisha mahakamani
Pia  wameharibu vibanda  vyote vilivyomo ndani ya misitu  na wamekamata Ng’ombe na  kutoza faini  na kisha wameziondoa katika misitu  ya Mkoa wa Katavi
  Alisema Wilaya ya Mpanda imeweka  utaratibu  wa kudhibiti  uvamizi  wa maeneo  ya hifadhi  unaofanywa  kwa kuweka  makazi ,kilimo  kuchungia mifugo  ujangiri wa  wanyama pori  na uvunaji  wa magogo  hususani  katika  maeneo  ya msitu  wa hifadhi  wa Tongwe mashariki ,Nkamba  na  ushoroba  wa wanyamapori  wa Lyamgoroka  na misitu  hifadhi   ya vijiji vya Mpembe na Katuma

No comments:

Post a Comment