Wednesday, December 16, 2015

CHADEMA KATAVI WAFUKUZA VIONGOZI WAO BAADA YA KWA TUHUMA ZA KUKISALITI CHAMA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
 Hari ya Chama cha Demokrasia (Chadema) Mkoani  katavi si shwari    hari iliyopelekea  viongozi wa  Chama hicho wa ngazi ya Mkoa na Wilaya  kusimamishwa uongozi  kwa kutuhumiwa kukisaliti  Chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu  wa Oktoba 25 mwaka huu
 Viongozi hao walisimamishwa uongozi  hapo juzi katika  mkutano wa kamati ya   mashauliano ya chama  hicho uliofanyika  katika ukumbi wa Katavi Resort  Mjini hapa na ulitawaliwa na vurugu kubwa  ya wafuasi   na wanachama waliokuwa wakishinikiza viongozi wao wajiuzuru
Viongozi waliosimamishwa na mkutano huo uliongozwa na  mtaribu wa Chadema wa Kanda ya Magharibi  Cristophar  Namwanji  ni Katibu wa   Bawacha  Hamisa  Korongo wa  Mkoa  na Mwenyekiti wa  Bavicha  Fransis  Misigaro
Viongozi  wengine waliosimishwa  ni  Mwenyekiti wa Chadema  wa Wilaya ya Mpanda  Abrahamu Mapunda  na  katibu wa Wilaya Idd Faraji pamoja na  Mwenyekiti  wa Bavicha  na Katibu wa  Bawacha wa Wilaya ya Mpanda
Mkutano huo pia umewasimamisha uongozi  viongozi wa jimbo la Mpanda Mjini  ambao ni  Mwenyekiti wa Jimbo la Mpanda Mjini  Braisoni Mwalugala   Katibu wa Jimbo hilo Patrick  Richald na  Katibu na Mwenyekiti wa jimbo wa Bavicha  na  Bawacha
Viongozi hao waliosimamishwa wanadaiwa kuwa walikiujumu chama hicho  wakati wa uchaguzi mkuu na kusababisha  chama  hicho kushindwa vibaya wakati  wa uchaguzi  mkuu uliofanyika hivi karibuni na kupoteza jimbo la Mpanda Mjini  liliokuwa lililoongozwa na Said  Arfi(Chadema) kwa kipindi cha miaka kumi
Mbali ya kusimamishwa uongozi viongozi hao wametakiwa kukabidhi mali zote za Chama  hicho zikiwemo pikipiki walizokuwa wakizitumia kufanyia  shughuli za  chama hicho
Mkutano huo  ulifanyika  huku   kukiwa na ulinzi  mkali wa polisi  waliokuwa wamevaa sare na wengine wasio   na sare wakiwa wameongozwa na mkuu wa  Kituo kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Mpanda kufuatilia kuwepo kwa dalili za kuwepo kwa vurugu kwenye mkutano huo
 Hivi  karibuni  wafuasi na wanachama wa  chama hicho walivamia ofisi za  Mkoa   kwa  lengo la kuwashinikiza viongozi hao wajiuzuru  kutokana na kukiujumu  chama  hicho
Kwa upande wake katibu wa  Chama  hicho wa Wilaya ya Mpanda Idd  Faraji  alisema kuwa   mkutano huo  haokuwa  halali  kwani  wajumbe  walioshiriki  kutowa maamuzi hayo hawakuwa ni wajumbe  halali wa mkutano huo

No comments:

Post a Comment