Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Jumla ya
wanachama 24 wa CCM katika
Mkoa wa Katavi wamerudisha fumu
za kuomba kuteuliwa kugombea
ubunge wa majimbo matano ya uchaguzi yalioko Mkoa wa Katavi kupitia CCM
Wagombea hao walirudisha fomu kwenye ofisi
za Wilaya zao
hapo juzi ambapo
ndio ilikuwa siku ya mwisho ya watu kurudisha fomu za kuomba kugombea
ubunge kwa ajiri ya kumpata mgombea
atakaye wakilisha chama hicho kwenye uchaguzi
mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu
Mkoa wa Katavi unajumla ya majimbo ya uchaguzi matano
ambayo ni Jimbo la Mpanda
Mjini , Mpanda Vjijini , Nsimbo ,
Kavuu na Jimbo la Katavi
Waliorudisha fomu kwa ajiri ya kugombea jimbo la Nsimbo ni
Said Amouri Arfi ,Richald Mbogo ,Hassanal Shabir Dalla ,Manamba David ,na
Frenk Mapesa
Waliomba kugombea
jimbo la Kavuu ni watatu ambao ni
Emanuel Zumba ,Mselem Said Abdalla
na Mbunge wa viti maalumu aliye
maliza muda wake Pudensiana Kikwembe
Jimbo la Katavi lina wagombea watano
Mwandisi Izack Kamwelwe, Maganga Kampala ,Leph
Gembe , Shafi Mpenda na Osca
Albano
Kwaupande wa jimbo la Mpanda Mjini
Katibu msaidizi wa CCM
Wilaya ya Mpanda Robart
Joseph aliwataja waliorudisha
fumu kuwa ni Gabriel Mnyere , Sebastiani Kapufi
na Galus Mgawe
Jimbo la Mpanda Vijini
ni Abdalla Sumry , Moshi
Kakoso , Chifu Charles Malack ,Godfrey Nkuba , Wiliam Makufwe, Elizabeth Sulutani
na Rock Mgeju
Kampeni za
kujinadi wagombea hao wa zilianza
jana kwenye majimbo ya Mpanda
Mjini na Mpanda
vijini
Kabla ya kuanza kwa kampeni hizo za kujinadi kilifanyika kikao
cha wagombea uchaguzi wa majimbo yote ambapo baadhi yao walitowa malalamiko ya
kuanza kuchezeana lafu kwa baadhi ya
wagombea wamekuwa wakitumia kampeni za udini
Uchunguzi
uliofanywa hivi karibuni na mwandishi wa habari hii hili
umeweza kubaini kuwa kumekuwa na tabia
ya baadhi ya wagombea hao kununua kadi za CCM
kutoka sehemu nyingine
hasa Dodoma na kuwaletea watu na
kuwagawa bure bila kujali itikadi za vyama vyao ili watu hao waweze kuwapingia kura maonikwenye mikutano mikuu ya Kata mbalimbali

No comments:
Post a Comment