Tuesday, March 24, 2015

TAASISI ZA SERIKALI ZATAKIWA KULIPA MADENI YAO YA MAJI

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Dk  Ibrahimu Msengi  ameziagiza Taasisi  za Serikali zilizopo  katika Mkoa wa  Katavi  ameziagiza  zihakikishe zinalipa  madeni yao makubwa  na yamuda mrefu  wanayodaiwa na Mamlaka  ya Maji safi na maji taka ya mji wa Mpanda (MUWASA) ili mamlaka  hiyo  iweze  kujiendesha
 Agizo hilo alili maadhimisho  ya kilele cha   cha   maadhimisho ya wiki ya maji  yaliofanyika kimkoa katika Kijiji cha  Ngoma lusambo Wilaya ya Mpanda katika hotuba yake  ilisomwa kwa niaba yake na Kaimu mkuu wa  Mkoa wa Katavi ambae pia   ni  Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali msitaafu  Issa  Njiku
 Alisema  mamlaka ya maji safi na maji taka ya mji wa Mpanda imekuwa  ikikwama kujiendesha kufanya baadhi ya shughuli zake kutokana  na madeni makubwa  ya fedha  ambayo  MUWASA  wanazidai  baadhi ya  Taasisi za Serikali zilizopo katika Mkoa wa Katavi kwa muda mrefu sasa  na huku wakiendelea kupatiwa huduma ya maji
 Alifafanua ili  Mamlaka hiyo ifanye shughuli zake vizuri  taasisi  zote  zote ambazo  zinadaiwa madeni makubwa ziakikishe zinalipa madeni hayo   haraka kwa MUWASA ili mamlaka hiyo iweze  kujiendesha
 Aliitaka  mamlaka ya maji safi na  maji taka ya  Mji wa Mpanda kuwa na utaratibu  wa kugawa maji  kwa  wananchi kwa uangalifu  na bila kuwa  na  upendeleo wowote kwa wateja wao
 Alitowa wito kwa  mamlaka  zinazosimamia  maji ziweke  mpango wa kuwapatia  wananchi maji  safi na salama  kwa gharama  nafuu
 Dk  Msengi alisema  kamati za maji  ziundwe kwenye kila Kijiji  na mtaa  ili kamati hizo  zifanye kazi ya  kusimamia maji  kwenye vijiji vyao na mitaa yao
 Alisema  kazi ya  usambazaji  wa maji  unaendelea  vizuri   kwani  asilimia  kubwa ya  wananchi wa  Mji wa  Mpanda  na Mkoa wa Katavi kwa ujumla wanapata maji safi na salama
Katika  maadhimisho hayo ya wiki ya maji  kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Kanali Mstaafu Issa Njiku alizindua mradi wa maji   katika Kijiji cha Ngoma Lusambo  uliogharimu kiasi cha shilingi  milioni 288 ulifadhiliwa na Benki ya Dunia  maradi huo ambao utawasaidia  zaidi ya wakazi 2000 wa kijiji hicho


    

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment