Sunday, March 22, 2015

Bodi ya maji ya bonde la ziwa Rukwa imewahamasisha jamii ya watu wanaoishi katika bonde godo la mto katuma Wilayani Mpanda


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Bodi ya maji ya bonde  la ziwa Rukwa  imewahamasisha  jamii ya watu  wanaoishi  katika  bonde godo  la mto katuma  Wilayani  Mpanda  Mkoa wa Katavi nanma ya  kusimamia na kulinda  rasilimali za maji
Viongozi wa Bodi hiyo  wamefanya  uhamasishaji kwa kwa  watu wa vijiji  nane  ambavyo  watu wake  ni watumiaji wa maji  ya bonde la  ndogo la mto Katuma wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji
Akizungumza na Wanachi wa Kata ya Mwamkulu  hapo jana  Afisa  mahusiano  toka bodi  ya maji  ya bonde la  ziwa Rukwa   Thadeus  Ndeseiyo  alisema bodi hiyo imekuwa  ikifanya  shughuli za  kusimamia  uhifadhi  wa mabonde madogo  ya mito iliyoko katika mikoa ya Katavi ,Rukwa   Mbeya  Singida  na Tabora chini ya ufadhili  wa  shirika  la GIZ  la nchi ya Ujerumani
 Alisema lengo la bodi hiyo ni  kuhamasisha  jamii iliyopo  katika bonde  la mto  Katuma na maeneo mengine  kusimamia  rasilimali za  za maji  ambazo siku hizi za karibuni zilikuwa zimeharibiwa 
 Alisema siku za hivi karibuni  mto  Katuma ambao  ni tegemeo kubwa la  maji  kwa wanyama wa hifadhi  ya mbuga ya Katavi  ambao wanayatumia maji  umekuwa na tabia ya kukauka mara kwa mara kutokana na uharibifu wa mazingira
Nae Afisa maendeleo   wa bodi ya bonde la ziwa Rukwa  Mgaujilwa  Watison  alieleza kuwa uhamasishaji huu wa kuelisha jamii nanma ya  kutunza na kulinda Rasilimali za maji ni zoezi endelevu
 Alisema   watu wanapaswa watambue  kuwa swala la kulinda na kutunza rasilimali za maji ni lalazima na sio jambo la hiari hivyo wananchi wanapaswa watambue hivyo
Mwenyekiti  wa umoja wa watumiaji wa Maji wa bonde la mto Katuma Gerald  Majura alieleza kuwa bado kuna changamoto ya watu  bado  hawajui  umuhimu  wa vyanzo vya maji
 Alifafanua kuwa wapo baadhi ya watu bado wanafanyia shughuli za kibinadamu  kwenye vyanzo vya maji  kwa  kufugia mifugo yao
Kwa upande  mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Mwamkulu Saimon  Gwambi alisema kuwa  tangu kuanzishwa  kwa jumuia ya watumiaji wa maji ya bonde dogo la mto Katuma hapo mwaka jana  faida zake zimeanza kuonekana
 Alisema Kwani uoto wa asili  ambao ulikuwa umeisha potea  umeanza kuonekana   baada ya watu kuelimishwa nanma ya kulinda  rasilimali za maji   hivyo hari ya mazingira imeanza kurudi  kwenye hari yake ya kawaida
Kaimu  Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Said  Mwapongo  alieleza kuwa  lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mtu anapata huduma ya maji  hivyo ni vizuri  rasimali za maji  vitunzwe vizuri ili maji yasije  yakakauka
Katika wiki hiyo ya maji  viongozi wa bonde la ziwa Rukwa  waliandaa mashindano ya mpira wa miguu yaliyowashilikisha timu za vijana kwalengo la kuwahamasisha  vijana namna  ya kuhifadhi  mabonde  na  vyanzo vya maji kupitia  mashindano hayo ya mpira wa mguu wa wanaume na wanawake kauli  mbiu ya maji mwaka huu  maji kwa maendeleo  endelevu
MWISHO

    

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment