Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Serikali imepanga kutoa ruzuku kwa wavuvi wa samaki ili
kuwawezesha wavuvi waweze kupata vyombo
bora vya uvuvi vitakavyowasaidia
kwa ajiri ya shughuli zao za uvuvi
ili weweze kununua zana bora ili
waondokane na uvuvi wa zana duni za uvuvi
Hayo yalisemwa hapo jana na Waziri wa
Maendeleo Mifugo na uvuvi Dr Titus
Kamani wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha
Ikola wakati wa ziara yake ya siku
mbili ya kukagua miradi mbalimbali inafanywa na Wizara hiyo Mkoani hapa
DR Kamani alisema
Serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta ya uvuvi imeamua
kuanza kutowa ruzuku kwa
wavuvi kama ambavyo inavyofanya kwa wazalishaji wa mazao mbaalimbali ya kilimo
Alifafanua
shughuli za uvuvi zimekuwa ni
tegemewa na watu wengi kwa ajiri ya kujipatia kipato chao ambapo
jumla ya watu zaidi ya milioni nne
wanajishughulisha na uvuvi na kuwa ndio sehemu yao ya kujipatia kipato
chao na ajira
Alisema
Serikali inatambua kuwa wananchi hawajanufaika
na kufaidika na uvuvi kutokana na kuendelea kutumia zana
duni kwenye shughuli zao za uvuvi
Dr Kamani alieleza katika kuhakikisha sekta ya
uvuvi inaendelea kukua hapa nchini Serikali
imeongeza vyuo vya wataalamu wa
samaki ili Serikali iweze kuwa na
wataalamu maalumu kwa ajiri ya
samaki tuu
Aliwata wavuvi wa samaki waanze kuwa na utaratibu wa kujiunga
na mifuko ya hifadhi ya jamiii
ambayo itawakopesha na kuwafanya waweze kununua zana bora za uvuvi na pia
waweze kujiwekea akiba yao ya uzeeni kwani
watakuwa wamejiwekea akiba yao pindi watakapo kuwa wamezeeka
Kwa hari hiyo
maafisa ushirika wafike kwenye maeneo ya wavuvi na kuwaelimisha namna ya
kuunda vikundi vya ushirika ambavyo
vitawasaidia kukopa kwenye mifuko
ya kijamii
Kwa upande Katibu
Tawala wa Mkoa wa Katavi Mwandisi Emanuel Kalobelo alisema
wavuvi wa samaki wa Mkoa wa
Katavi wamefanikiwa kuongeza matumizi ya zana bora za uvuvi
kutoka boti za injini
290 julai 2013 hadi boti za
injini 385 Desemba 2014 sawa na ongezeko la asilimia 25
Aidha Mkoa wa Katavi umetowa mafunzo ya elimu ya uvuvi
kwa wavuvi 2,420 kwa mwaka 2014
yatakayowasaidia kupata maarifa ya uvuvi
ukilinganisha na mwaka 2013 ambapo
wamafunzo yalitolewa kwa wavuvi 812
Mwandisi Kalobelo alisema Halmashauri ya
Wilaya ya Mpanda kwa mwaka wa fedha wa
2014 na 2015 imetenga kiasi cha shilingi milioni 40 imetenga kwa ajiri ya kununua boti
za uvuvi ambapo hadi sasa injini mbili
aina ya Yamaha zenye ukubwa
wa 40 HP zimenunuliwa
Alisema ni matarajio ya Mkoa kuwa
uwepo wa boti hizo utapunguza kwa kiasi
kikubwa uwepo wa uvuvi
haramu katika Ziwa Tanganyika
Alifafanua
Mkoa wa Katavi katika kutekeleza
sera na mkakati
wa Taifa wa sekta ya uvuvi ya
mwaka 1997 pamoja na sera ya uvuvi
ya mwaka 2003 umehamasisha
wananchi kufuga samaki ili kuboresha
afya na kupunguza umasikini
wa kipato
Alisema
hadi kufikia desemba mwaka jana
mkoa wa Katavi ulikuwa na jumla ya mabwawa hai 60
ya kufungia samaki yalioanzishwa na wafugaji binafsi ukilinganishwa na mabwawa
51 ya mwaka 1013 hili ni sawa na ongezeko la asilimia 15
Alieleza
pamoja na ongezeko hilo Mkoa
unakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa kituo cha kuzalisha mbegu
bora za vifaranga
vya samaki jambo lililosababisha wafugaji wengi kushinnnnnnnnndwa kupata mbegu bora
ya samaki
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment