Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Wiara ya Mifugo na imeziagiza Halmashauri zote
hapa ncini kuacha mara moja kufanya
minada ya mifugo kwenye minada yote
ya kuuza mifugo ambayo haina mizani ya kupimia mifugo
Agizo hilo limetolewa hapo jana na Waziri wa Maendeleo
ya mifugo na uvuvi Dr Titus
Kamani wakati alipokuwa
akizungumza na viongozi wa Mkoa
wa Katavi na wafugaji na pamoja
na wavuvi katika katika ukumbi
wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Katavi
Alisema
wafugaji wamekuwa hawanufaiki na
mifugo yao wanayoiuza kutokana na kuuza
mifugo yao bila kupimwa kwenye
mizani kutokana na maeneo mengi
ya minada inayomilikiwa na Halmashauri kutokuwa na na mizani ya kupimia uzito wa mifugo
Dr
alieleza Serikali imeagiza
kuanzia sasa maeneoo yote ya minada yawe na mizani ya kupimia mifugo ilikumfanya mfugaji afahamu uzito wa mifugo
yake inauzito wa kiasi gani na
aweze kuuza kulingana na hari halisi ya uzito wa mifugo yake na kumfanya mfugaji anufaike
Alifafanua
kuwa mazao mengine
yote yanayouzwa kwenye minada hapa nchini wafanyabiashara uuza zao yao
yote hupimwa kwa mizani kwanini na mifugo nayo isipimwe kwenye mizani
alisema Waziri Kamani
Alisema hari hiyo ya wafugaji
kutouza mifugo yao kwa kupima
kwenye mizani kumewafanya baadhi
ya wafugaji wengine kukata tamaa
ya kujishughulisha na maswala ya ufugaji wa mifugo
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Katavi katika
taarifa aliyoisoma ya sekta ya mifugo
alieleza kuwa Mkoa wa Katavi unajumla ya Ng’ombe 244,009 mbuzi
120,000 kondoo 43,358 hata hivyo
ufugaji huo wa mifugo
haufanyiki kisasa kwa hari hiyo Mkoa unalo jukumu
hili la kuendeleza sekta ya mifugo
Alisema mkoa umetowa mafunzo kwa wafugaji 4,591kwa kipindi cha mwaka 2013 na mwaka 2014 ambao wamepatiwa mafunzo
juu ya ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa na nyama vikundi vitatu vimepata mafunzo ya uchakataji wa ngozi
wafugaji 10 wamepatiwa mafunzo
ya uendeshaji wa ranchi katika Ranchi ya Kalambo Mkoani Rukwa na wafugaji
215 wamepata mafunzo ya ufugaji
bora wa kuku wa asili
Mwandisi Kalobelo alieleza Mkoa wa Katavi
unakabiliwa na changamoto ya upungufu
wa wataalamu wa mifugo ambapo kwa sasa inao wataalamu 27
wakati wanaohitajika ni wataalamu 67
hivyo kuna upungufu wa wataalamu 40 wa
mifugo katika Mkoa huu
Alitaja changamoto nyingine kuwa ni uhaba
wa vitendea kazi kama vile
vyombo vya usafiri magari ,pikipiki kwa ajili ya
matumizi ya shughuli za kiutendaji
wa sekta hiyo ya Mifugo katika mkoa wa Katavi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment