Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mamlaka ya Rufaa
ya Zabuni za Umma (PPAA) imetowa mafunzo ya
uelimishaji kuhusu Sheria
mpya ya ununuzi wa Umma na taratibu
ya uwasilishaji wa
malalamiko kama zilivyo ainishwa katika
sheria mpya ya ununuzi
wa Umma ya mwaka 2011 kwa wajumbe wa Bodi za zabuni Maafisa
ugavi wa Mkoa wa katavi na Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi makandarasi na wazabuni
Semina hiyo ya siku mbili ilifunguliwa hapo jana na Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe
ambae ameamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga
kwenye ukumbi wa chuo kikuu Huria cha Mkoa wa Katavi
Katika hotuba yake ya ufunguzi Dr Rutengwe
aliwaeleza washiriki wa semina hiyo kuwa
ni vema watambue kwamba ununuzi
wa umma
ni moja kati ya
maeneo muhimu katika
utendaji wa Serikali kwani zaidi ya asilimia sabini ya bajeti ya nchi
inagusa manunuzi
Alisema mafunzo hayo
ni muhimu kwani yatawasaidia washiriki hao
kufahamu sheria mpya ya ununuzi
wa umma
Namba 7 ya mwaka 2011 na taratibu
za utatuzi wa migogoro itokanayo na ununuzi wa Umma
Alifafanua Serikali imeweka chombo cha
Mamlaka ya Rufaa ya manunuzi ya Umma (PPAA)
ili kuweza kuwasaidia watu wakate rufaa pale ambapo
wanapoona haki haija tendeka
Alisema Mamlala
ya Rufaa ya Zabuni za umma
ni chombo cha Serikali
chenye dhamana ya kupokea na kutatua migogoro
itokanayo na ukiukwaji
wa taratibu za ununuzi
wa umma kama zilivyoanishwa katika
sheria ya ununuzi wa
Umma ya mwaka 2011
Dr
Rutengwe alieleza lengo kuu la kuanzishwa kwa mamlaka
hii ni kuwa chombo ambacho
kitatatua migogoro itokanayo
na ununuzi wa Umma nje ya mahakama ilikutochelewesha utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya Serikali
ambayo ni muhimu
kwa maendeleo ya Nchi
Kwa upande wake
mwanashria wa PPAA Florida Mapunda
aliwaeleza washiriki wa semina hiyo kuwa sheria hiyo Mpya namba 7 ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 imanza
kutumika Desemba 20 mwaka jana
Alisema
kabla ya mwaka 2001 Tanzania
haikuwa na mfumo
rasmi wa sheria wa ununuzi wa Umma wala
chombo mahsusi cha kudhibiti
hivyo mfumo na taratibu za ununnuzi wa umma zilitofautiana na
hazikuwepo taratibu maalumu za
uwajibikaji
Aliwafafanuliwa
washiriki hao kuwa mpaka sasa mamlaka hiyo ya Rufaa ya manunuzi za umma
imeisha pokea kesi za rufaa miambili na arobaini
Nae
Kaimu katibu mkuu wa (PPAA)
Mbile Kissiok alisema kuwekupo na
malalamiko mingi ya watu wanaokuwa
wameomba tenda mbalimbali kutokana na
kutofahamishwa kwa matokeo ya tenda
wanazokuwa wameomba
Alisema ni wajibu kwa maafisa ununuzi kuwapatia taarifa ya matokeo ya mshindi
wa tenda hata kama aliyeomba tenda anapokuwa ameshindwa badala ya kutoa taarifa kwa mtu aliyeshinda tenda tuu
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment