Na Walter wa Katavi yetu
MWANAFUNZI, Jenifa Leonard (17) aliyekuwa akisoma katika
shule ya Msingi Shanwe, Halmashauri ya Mji wa Mpanda, amejiuwa kikatili baada ya kubaini kuwa amefeli
mtihani wa kumaliza elimu ya
msingi mwaka huu .
Habari kutoka eneo
la tukio zimebainisha kuwa marehermu
alikunywa dawa za aina mbalimbali akitumia mafuta ya taa baada ya kukasilishwa
na matokeo yake ya kufeli mtihani wa darasa la saba.
Kwa mujibu wa
akaka yake , Masumbuko Leonard ,
marehermu alifariki usiku wa kuamkia jana majira ya saa nane na nusu usiku muda
mfupi baada ya kufikishwa katika Hospital ya Wilaya ya Mpanda kwa matibabu
Alisema siku hiyo ya tukio marehemu ambae
amemaliza darasa la saba mwaka huu Katika Shule ya Msingi Shanwe
pamoja na mdogo wake aitwaye Jackilina Wiliamu walikuwa wamekaa
nyumbani ndipo walipoletewa taatifa ya matokeo ya darasa la saba na
mwanafunzi waliemaliza nae shule moja .
Alisema mwanafunzi huyo
alimweleza marehemu na mdogo wake kuwa matokeo ya ufaulu wa darasa
la saba yaliotangazwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yameonyesha kuwa marehemu
amefeli ila mdogo wake Jackilina yeye amefaulu mtihani
huo.
Baada ya kuambiwa hivyo marehemu hakuamini aliamua kwenda
kwenye mtandaa ili aweze kuhakikisha kama kweli amefeli mtihani wa kumaliza
darasa la saba na alifika huko alikuta matokeo ni kama alivyokuwa
ameambiwa ya kuwa amefali
Alieleza marehemu Jenifa kisha alirudi
nyumbani na kumkuta mdogo wake ambae yeye amefaulu na alimweleza
kuwa anaona aibu yeye mkubwa kufeli na mdogo wake amefaulu hivyo ni
bora anywe sumu
Alisema aliendelea kumweleza mdogo wake
kuwa anamtakia aendelee na masomo vizuri na maisha ya hapa
duniani kwani yeye na mdogo wake hawata onana tena Dunia kwani yeye
anatangulia mbele za haki
Masumbuku alieleza kisha marehemu aliingia ndani ya
chumba cha mama yake aitwaye Stela Joseph ambae muda huo hakuwepo
nyumbani na ndani ya chumba hicho kulikuwa na dawa za binadamu za aina
mbalimbali ndipo alipozichukuwa na kuzinywa kwa kutumia mafuta ya taa
Alisema kisha alitoka sebuleni na kumkuta
Jackilina na alimweleza kuwa tayari ameisha kunywa dawa kwa
kutumia mafuta kutokana na kukasilishwa na matokeo yake ya darasa la saba hata
hivyo Jackilina alifikiri dada yake anamtania
“ Baada ya muda marehemu alianguka chini na kumfanya Jackilina akote nje na kukimbia kwenda kuomba
msaada kwa majirani ambao walimkimbiza katika Hospitali
ya Wilaya ya Mpanda hata hivyo ilipofikia majira ya saa nane
na nusu usiku akafariki dunia
mwili wa marehemu
umehifadhiwa katikachumba cha kuifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya
Mpanda na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya Shanwe ‘
alibanisha
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashi amethibisha kutokea kifo cha mwanafuzi huyo na
jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na kifo hicho
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment