Sunday, August 10, 2014

DC MPANDA AWAAGIZA WAKURUGENZI KUTEKELEZA MAAGIZO YAKE‏

Na  Walter  Mguluchuma  
Mpanda Katavi
Mkuu wa Wilaya  ya Mpanda  Mkoa wa Katavi   Paza  Mwamlima amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na  wa Mji wa Mpanda kuhakikisha   wanatekeleza agizo lake alilolitoa la kuwasaka  na warudisha  mashuleni  wanafunzi wote walioacha masoma na kukimbilia kuolewa na kuowa

Mwamlima alitowa maagizo hayo ya kuwataka wakurugenzi walioko kwenye Wilaya yake   watekeleze maagizo yake  hapo juzi wakati akiwa ofisini kwake kwenye kikao chake na wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  na Mji  wa Mpanda  kikao hicho kiliwashirikisha wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama  wa Wilaya ya Mpanda
Alisema kumekuwepo na tatizo kubwa la  wanafunzi  kukatisha masomo  kwa  lengo la kuolewa na wengine kwa ajiri ya kuowa kitendo hicho  ambacho  hakitakiwi  
Alifafanua kutokana na kushamiri kwa utoro wa wanafunzi  alilazimika kutowa agizo  hapo  mwezi mei  mwaka huu wakati alipofanya ziara kwenye shule ya Sekondari ya Mpanda Ndogo alipokuta zaidi ya nusu ya  wanafunzi wa shule hiyo walikuwa wameacha masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya wanafunzi kuolewa
 Wakati wa  ziara yake  hiyo  alishitushwa na taarifa ya kutoripoti shuleni wanafunzi wawili wa shule ya Msingi Vikonge ambao waliongoza kwa matokeo ya ufaulu wa mtihani wa kumaliza  Darasa la saba mwaka  jana   lakini wameshindwa  kujiunga na kidato cha kwanza katika Sekondari ya  Mpanda Ndogo
Dc  Mwamlima  kwenye ziara hiyo aliwaagiza wazazi wa wanafunzi  walioacha masomo wahakikishe wanawarudisha shuleni watoto wao hata kama wameulewa na kuzaa watoto
Pia aliwaagiza wakurugenzi hao wahakikishe wanafanya kikao cha pamoja baina ya Halmashauri hizo  na   Hifadhi ya Taifa ya Katavi  na Vijiji vinavyozunguka hifadhi ili kuonyesha mipaka  kwa lengo la kuondoa migogoro  baina ya vijiji na Hifadhi
Aidha amewaagiza  waandae  kikao  cha pamoja  cha wadau wa mto Katuma  ili waweze  kujadili na kupanga mikakati ya kuunusuru mto huo usikauke ambao  ni tegemeo la wanyama waliooko kwenye Hifadhi ya Katavi
Amewaagiza vilevile wamalize  ujenzi wa maabara kabla ya mwezi wa tisa mwaka huu  ili nayeye  aweze kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais alilolitowa la kila shule ya Sekondari hapa Nchini lazima iwe na jengo la maabara


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment