Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya (DC) ya Mpanda mkoani Katavi, Paza Mwamlima
amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za Mpanda na Mji wa Mpanda
kuhakikisha wanatekeleza agizo lake la kuwasaka na warudisha shuleni
wanafunzi walioacha masoma na kuozwa.
Mwamlima alikazia agizo hilo juzi wakati akizungumza na wakurugenzi
hao katika kikao kiliwashirikisha wajumbe wa kamati ya ulinzi na
usalama wa wilaya ya Mpanda.
Alisema kuwa kumekuwepo na tatizo kubwa la wanafunzi kukatisha
masomo kwa lengo la kuolewa na wengine kwa ajiri ya kuowa, jambo
alilosisitiza kuwa ni makosa.
Alisema kuwa Mei mwaka huu, alifanya ziara kwenye shule ya sekondari
ya Mpanda Ndogo ambapo alikuta zaidi ya nusu ya wanafunzi wameacha
masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kuolewa.
Katika ziara hiyo, aliwagiza wazazi wa wanafunzi walioacha masomo
wahakikishe wanawarudisha shuleni watoto wao hata kama wameolewa na
kuzaa.
Pia aliwataka wakurugenzi hao wahakikishe wanafanya kikao cha pamoja
baina ya halmashauri hizo na Hifadhi ya Taifa ya Katavi pamoja na
vijiji vinavyozunguka hifadhi ili kuonyesha mipaka kwa lengo la kuondoa
migogoro baina ya vijiji na Hifadhi.
Mkuu huyo, pia aliwaagiza wakurugenzi hao waandae kikao cha
pamoja cha wadau wa mto Katuma ili waweze kujadili na kupanga mikakati
ya kuunusuru mto huo usikauke kwa kuwa ni tegemeo la wanyama wa Hifadhi
ya Katavi.
Chanzo:Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment