Jiunge na Huduma ya Tone Mobile News Bure kabisa kupitia Whatsapp yako na uwe wa kwanza kupata kile kinachotokea ni Rahisi sana Ingia katika uwanja wa kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika Whatsapp yako kisha andika TONE MOBILE NEWS tuma kwenye namba 0756364660 utapokea ujumbe kuwa umeunganishwa.
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi imefanikiwa kukusanya mapato ya ushuru wa ndani jumla ya shilingi Tsh 753,042,184 kwa kipindi cha june 2013 hadi june 2014 ikiwa ni asimia 105.6 ya lengo la makusanya waliokuwa wamepanga kukusanya
Hayo yalisemwa hapo jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo Neneka Rashid wakati wa Mkutano mkuu wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo uliofanyika katika ukumbi wa Hakmashauri hiyo
Rashid alisema Halmshauri hiyo ilikuwa imeweka lengo la kukusanya mapato ya Tsh 713,328,000 lakini imeweza kuvuka lengo kwa kukusanya kiasi cha Tsh 753,042,184 ambazo ni sawa na asilimia 105.6
Alifafanua kutokana na kukusanya kiwango hicho cha mapato ya ndani Halmashauri hiyo imewaza kuvuka lengo walilokuwa wamepanga kwa kiwango cha asilimia 5.6
Alitaja sababu zilizofanya Halmashauri hiyo kuvuka lengo la makufanyo kuwa Halmshauri iligawanya vyanzo vya mapato yaani mazao ya kilimo na magulio kwa eneo moja
Pia walifanya ukaguzi wa mara kwa mara wa kuwakagua mawakala na waliweza kutoa maelekezo kwa mawakala pale palipohitajika na mawakala walifuata maelekezo hayo
Alisema Halmashauri imefanikiwa kuweza kujibu hoja zote za ukaguzi wa ndani na za nje imeweza kuzijibu kwa wakati pale walipotakiwa kufanya hivyo
Rashid alitaja baadhi ya changamoto zinazokabili Halmashauri hiyo kuwa ni migogoro ya mara kwa mara baina ya Madiwani na watendaji wa Halmashauri
Changamoto nyingine ni watendaji wa vijiji na Kata kutoitisha vikao vya kikatiba kwenye maeneo yao na kusababisha wananchi kutosomewa mapato na matumizi na kuwafanya wananchi kutokuwa na imani na viongozi hao na kuwavunja moyo wananchi wa kujitokeza kwenye shughuli za kujitolea
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Machimboni Raphael Kalinga aliomba Halmshauri hiyo iwe inaweka wazi mikataba ya wakandarasa kwenye eneo la mradi husika kwani mikataba mingi imekuwa ni yasiri
Alisema endapo mikataba itakuwa wazi kwa madiwani itawafanya waweze kuisimimia miradi inayojengwa kwenye kata zao kwa ukalibu zaidi
Nae afisa wa Serikali wa Mitaa wa Mkoa wa Katavi Lauteri Kanoni aliita Halmashauri hiyo kuendelea kubuni mapato mengine yatakayoiongezea Halmashauri ya Nsimbo mapato yao
Alieleza utaratibu wa kukusanya mapato unaweza kubadilika wakati wowote kwani baadhi ya mapato yanaweza yakabadilishiwa utaratibu badala ya kukusanya na Halmashauri yakakusanywa na Serikali kuu hivyo wasitegemee sana ushuru wa zao la Tumbaku ambao ndio unaoingiza ushuru mkubwa kwenye Halmashauri hiyo
Alisema katika Halmashauri nne zilizopo katika Mkoa wa Katavi ni Halmashauri mbili ambazo zimeweza kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani alizitaja Halmashauri hizo kuwa ni Nsimbo na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment