Friday, May 9, 2014

WAKAZI WA KIJIJI CHA SUNGAMILA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA BENKI YA DUNIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Walter  Mguluchuma
 Zaidi ya Wakazi  elfu moja wa Kijiji cha Sungamila Kata ya Kasokola Wilaya  ya Mlele  Mkoa wa Katavi  watanufaika na mradi   wa maji  unaofadhiliwa  na   Benki ya  Dunia  mradi ambao utagharimu  shilingi  milioni  mia mbili
Hayo  yamelezwa na  Diwani wa Kata ya Kasokola Crisanti   Mwanawima  hapo jana wakati  akizungumza  na mwandishi wa habari  kwenye ofisi yake ya Kata  iliyopo katika Kijiji  cha Kasokola
Alisema kijiji hicho  chenye jumla ya wakazi elfu moja na miambili  wanatarajiwa kunufaika na mradi huo   unaogharamiwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya shilingi milini  miambili  unatarajiwa kukamilika  hapo mwakani
Alifafanua kuwa mradi huo ulianza hapo   mwaka 2011 kwa hatua ya uchimbaji wa mitalo ya  kuwekea  mbomba  na mwezi ujao  shughuli ya ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji unatarajiwa kuanza mwezi ujao
Mwanawima alisema  mradi huo utakapokuwa umekamilika utasaidia kuondoa tatizo la maji Kijijini hapo  kwani Kijiji hicho  kinakabiliwa na tatizo la  uhaba wa maji kwani kijiji hicho  kina visima vifupi viwili tuu vinavyo  towa huduma ya maji kwa  wakazi wa Kijiji  cha Sungamila
Alisema  lengo la mradi huo   utakapo kuwa umekamilika ni  kusambaza  maji  kwenye baadhi ya vijiji vinavyo  zunguka Kijiji cha Sungamila  kutokana na kiwango  kikubwa  cha maji kitakacho kuwa kinapatikana
Mbali ya Kijiji  hicho   pia vijiji viwili vilivyopo kwenye Halmashauri ya Nsimbo Wlaya   ya  Mlele   navyo vitanufaika na mradi kama huu unaofadhiliwa na Benki ya Dunia vijiji  hivyo ni  Kapalala  na Isinde 

No comments:

Post a Comment