Wednesday, May 7, 2014

AFA BAADA YA KUNYWA VIROBA VYA ZED KUPITA KIASI BILA KULA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la  Michael Silanda (26 ) Mkazi    wa Kijiji  cha Ibindi  Tarafa ya Nsimbo  Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amefariki Dunia  baada ya kunywa Pombe (VIROBA )  aina ya Zed  kupita kiasi bila kula
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa Kamishina msaidizi  mwandamizi  Dhahiri Kidavashari  tukio hilo lilitokea hapo  mei tano mwaka huu majira ya saa sita usiku  kijijini  hapo
Alisema  siiku hiyo ya  tukio  marehemu baada ya kuamka  asubuhi  nyumbani kwake hapo majira ya saa tano  asubuhi  alielekea  kwenye  Bar ambayo ilikuwa ikiuza  vinywaji vya aina mbalimbali vya pombe  kali   na vinywaji baridi
Alifafanua kuwa baada ya kufika kwenye Bar hiyo aliwakuta  baadhi ya wanakijiji wenzake  wakiwa  wanakunywa pombe za aina mbalimbali  hari ambayo ilimfanya marehemu aweze kujumuika  nao  kwa kuagiza pombe (VIROBA  ) aina ya Zed
Alisema  Michael  aliendelea kunywa viroba  kuanzia  muda huo   kwenye bar hiyo bila kula kitu chochote  hadi  hapo  majira ya saa  sita  usiku  alipoamua kurudi  nyumbani kwake huku akiwa amelewa pombe  kupita kiasi
Baada ya kufika nyumbani kwake aliingia ndani ya nyumba yake  na kulala bila kula chakula chochote   na siku iliyofuata majira ya saa mbili asubuhi   ndipo  walipomkuta Michael  akiwa amefariki Dunia huku akiwa amelala kitandani kwake
Kamanda Kidavashari  alisema uchunguzi wa awali oliofanywa  kuhusiana na kifo hicho umebaini  kuwa kifo hicho kimesababishwa   na marehemu kunywa pombe nyingi kupita kiasi  bila kula  chakula
Alisema  mwili wa marehemu Michae Silanda umehifadhiwa kwenye chumba cha kuifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya kufanyiwa uchunguzi wa Kidaktari  na baada ya uchunguzi huo watakabidhiwa ndugu wa marehemu kwa ajiri ya  utaratibu wa mazishi

No comments:

Post a Comment