Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Jeshi la Polisi
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi linamshikilia Shabani
Hamad (48) Mkazi wa Mtaa wa
Mpanda Hoteli mjini hapa kwa kutuhumiwa kukamatwa na fedha noti bandia kiasi cha shilingi laki moja
Kamanda wa Jeshi
la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema mtuhumiwa Shaban alikamatwa na fedha hizo noti
bandia hapo Mei 24 mwaka huu majira ya saa kumi jioni katika
eneo la Mtaa wa Mpanda hoteli Mjini hapa
Mtuhumiwa huyo
kabla ya kukamatwa siku moja kabla ya tukio hilo la kukamatwa yaani mei 23
alikwenda kwenye kibanda kinachotowa huduma ya M-PESA kilichoko
katika mtaa wa Kawajense na alimkuta
muhudumu wa kibanda aitwaye Maria Joseph
na kumuomba ampatie huduma ya kuweka fedha kiasi cha shilingi laki moja
kwenye simu yake mkononi
Kidavashari
alifafanua baada ya mtuhumiwa
Shabani kukabidhi kiasi hicho cha
fedha kiasi cha shilingi laki moja za
noti za shilingi elfu mbilimbili mhudumu wa
kidanda hicho alimwingizia fedha kwenye
akaunti ya simu yake na kisha mtuhumiwa aliondoka kwenye eneo hilo
Alisema mara baada ya muda mfupi mhudumu wa kibanda
alianza kuzipanga fedha hizo na ndipo
aliposhituka alipoona namba za noti hizo
zinafana hari ambayo ilimfanya
awape taarifa wafanya biashara wenzake waliokuwa kwenye eneo hilo na
juhudi za kumsaka mtuhumiwa zikaanza hata hivyo hawakuweza kufanikiwakumpata kwani mtuhumiwa alikuwa ametokomea kusiko
julikana
Alieleza ndipo
mhudumu wa kibanda hicho cha M-PESA alipoamua kwenda kutowa taarifa kwa jeshi
la polisi kituo cha Wilaya ya Mpanda kuhusiana na tukio hilo
Baada ya taarifa
hizo jeshi la polisi lilianza msako wa
kumtafuta mtuhumiwa ambapo
waliweza kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa
akiwa katika eneo la mtaa wa mpanda hoteli akiwa na notinyingine bandia
za shilingi elfu mbili mbili zenye thamani ya shilingi laki moja ambazo
alikuwa amezichanganya na noti nyingine ambazo ni harali
Kamanda
Kidavashari alieleza kuwa Mtuhumiwa alikamatwa nabaadhi ya noti hizo
bandia zenye namba CK 194915 noti 20
Ck 1942911 noti 9 Ck 1942955 noti 11
Mtuhumiwa
anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati
wowote mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kuhusiana na tukio hili
kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi ametowa wito kwa wananchi wa Mkoa huu kujiadhari na
matapeli wanaozagaza noti bandia hasa katika kipindi hiki cha mavuno
na mauzo ya mazao mbalimbali
No comments:
Post a Comment