Saturday, May 31, 2014

DC MPANDA KUENDESHA MSAKO WA WANAFUNZI WALIOACHA MASOMO KWA UTORO NA WALIOOWA NA KUOLEWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  Paza Mwamlima amewaagiza  wazazi wa Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya  Mpanda Ndogo iliyoko  Tarafa ya Kabungu  Wilayani Mpanda  kuhakikisha  watoto wao  walioacha  shule kwa ajiri ya otoro na  kwa kwasababu ya kuowa na kuolewa  wahakikishe watoto wao   wanarejea shuleni  hata kama  wamezaa watoto
Mkuu huyo wa Wilaya alitowa agizo hilo  hapo juzi wakati  wa  mkutano  wa kamati ya maendeleo  ya Kata hiyo  pamoja na wazazi wawanafunzi wa  wanaosoma kwenye shule hiyo  ulifanyika shuleni hapo  kwa lengo la kujali maendeleo ya shule hiyo ambayo  ilishika nafasi ya mwisho  kwa ufaulu wa wanafunzi katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana kwa shule za sekondari za Mkoa wa Katavi
Alisema shule hiyo imekuwa na matokeo mabaya ya ufaulu  wa wanafunzi  kutokana  na utoro  uliokithiri  kwa  wanafunzi  kuacha shule  kwa ajiri ya kuowa na kuolewa huku wazazi wao wakiona kuwa ni jambo la kawaida
Mwamlima  aliwaeleza Serikali ya Wilaya  amepanga  kuendesha msako kwa kutumia jeshi la polisi  mwezi Julai  kuwasaka na kuwakamata na kuwapeleka shuleni wanafunzi wote watoro  na walioacha shule kwa kuowa na kuolewa hata kama watakuwa wamezaa watoto  watapelekwa shule na watoto wao migongoni
Alisema ni vizuri wazazi watowe ushirikiano katika zoezi hili ilikuweza  kuipandisha shule hiyo  na kuifanya ishike nafasi ya juu kwa ufaulu wa wanafunzi  kwani bila elimu  wazazi wa wanafunzi hao wataendelea kuwa masikini tuu   aliwaeleza Mwamlima
Awali  Mkuu wa Shule hiyo  Rashid  Msyete alieleza kuwa shuhttps://draft.blogger.com/blogger.g?blogID=2686366488337348656#editor/target=post;postID=5788232012877525037le hiyo yenye kidato cha kwanza hadi  cha nne  inawafunzi 165  kati yao  wanaume ni 104  na wanawake 61  wakati uwezo wa shule hiyo ni kupokea wanafunzi  600
Alisema kila mwaka shule hiyo inapangiwa kupokea wanafunzi 120 kwa ajiri ya kujiunga na kidato cha kwanza lakini wengi waao hawaripoti shuleni kutokana na  mwamko mdogo wa wazazi katika swala zima la elimu na kupelekea baadhi ya wazazi kuwaruhusu watoto wao kuolewa na kuowa
Kwa upande wake  mmoja wa wazazi  wa wanafunzi  Cristopha  Mkula  alisema kuwa  wanafunzi wanao soma kwenye Sekondari hiyo walikuwa wanakatishwa tamaa  kutokana na shule hiyo kuwa na waalimu wachache  hari ambayo ilisababisha wanafunzi  kukosa baadhi ya masomo na kuwafanya wawe watoro
Nae  Verovika  Godfrey  alieleza kuwa wanafunzi wengi wa shule hiyo wamekuwa ni watoro kutokana na adhabu  kali zinazotolewa na waalimu shuleni hapo pindi mwanafunzi anapokuwa amefanya kosa
Alisema ipo adhabu moja inayoitwa kunyonya mafuta  ndio imekuwa kikwanza kikubwa kwa wanafunzi kuwa  watoro shuleni hapo kwani huwa inatolewa kwa muda  mrefu kwa mwanafunzi
Hata hivyo mkuu wa wilaya Paza Mwamlima alimtaka mwanafunzi mmoja atowe ufafanuzi  wa aina ya adhabu hiyo ya kunyonya mafuta ni ya nanma gani ndipo mwanafunzi huyo alipo eleza kuwa edhabu hiyo  huwa ni ya mwafunzi huwa anaambiwa   aweke  kichwa chini ya ardhi   huku miguu ikiwa  ijuu
Aidha diwani wa Kata hiyo Hamad Mapengo alieleza kuwa  lile tatizo la upungufu wa waalimu  lililokuwepo awapo awali  mwaka huu limepungua sana baada ya Serikali  kupeleka waalimu  mapema mwaka huu

No comments:

Post a Comment