Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mahakama ya
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu
Wiliamu George 32 Mkazi wa Mtaa
wa Nsemlwa Wilaya ya Mpanda kifungo cha miaka 30
jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti kijana mwenzie 22 Mkazi wa Mtaa wa Mpandahoteli baada ya
kumnywesha pombe ya kienyeji kupita kiasi
Hukumu hiyo
ilitolewa hapo jana
na Hakimu mkazi
mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya
Mpanda Chiganga Ntengwa nahukumu
hiyo kuvuita hisia za watu
mbalimbali wa maeneo ya mjiwa Mpanda na Mkoa wa Katavi
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu wa mahakama
hiyo baada ya mahakama
kuridhika na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo
wa upande wa mashitaka na upande wa
utetezi
Katika kesi hiyohapo
awali mwendesha mashita mkaguzi wa jeshi la polisi Ally Mbwijo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa
alitenda kosa hilo hapo Novemba
21 mwaka jana majira ya kumi na
mbili jioni katika mtaa wa Mpanda Hotel
Mshitakiwa siku
hiyo ya tukiokabla ya kutenda
kosa hilo la kumlawiti
kijana huyo alidaiwa kunywesha pombe ya kienyeji aina ya komoni
walikuwa wakichanganya na bia nyumbani kwa mwamke aliyekuwa akiwauzia
pombe aliyetambulika kwa
jina moja la Lita katika mtaa huo wa Mpanda hotel
Ilielezwa na
mwendesha mashita Ally Mbwijo kuwa mshitakiwa
baada ya kuona mwenzake
ametoka anatoka njekwenda
kujisaidia alimwagiza dukani Lita
aende akamnulie sigara
Aliileza mahakama
baada ya kijana huyo ambaejina lake limehifadhiwa kurudi
ndani aliendelea na kunywa pombe
ambayo alikuwa ameisha kwenye chupa yake na
ndipo alipoteza fahamu na mshitakiwa alitumia nafasi huyo
kumwingilia kinyume cha maumbile
yakehuku akiwa amemlaza kwenye kochi
Mwendesha mashita
alieleza Lita alipotoka
dukani alimkuta mshitakiwa akiwa amekaa karibu na kijana
huyo ambae alikuwa amevuliwa nguo yake ya saruali
na akiwa akitambui na sehemu zake za
matakoni zikiwa zikiwa na mbegu
za kiume
Mshitakiwa baada ya kufanya kitendo hicho siku iliyofuata alimtuma
mama yake mzazi aende kwa jinana
huyo akamwombee samahani kwa kile alichoeleza
kuwa anahofia kufungwa jela
Baada ya mama
mshitakiwa Wiliamu George
kumwombea msamaha kwa kijana alilawitiwa
alikubali kumsamehe mshitakiwa
kwa kuhofia kupata aibu
Mshitakiwa baada
ya kusamehewa alianza kumtangaza kijana huyo
kwa rafiki zake na kuwafahamisha kuwa kijana huyo ni shemeji yao
kitendo ambacho kilimkasilisha kijana
huyo na kuamua kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ya kulawitiwa kwake na Mshitakiwa Wiliamu George
Hakimu mkazi
mfawidhi Chiganga Ntengwa kabla ya kutowa hukumu hiyo aliiambia mahakama kuwa mahakama imemtia hatiani mshitakiwa Wiliamu
George kwa kosa la kumwingilia
kijana huyo kinyumbe na maumbile
yake hivyo mahakama inatowa na fasi kwa mshitakiwa kama anasababu ya msingi ya
kuishawisha mahakama impunguzie adhabu aieleza mahakama hiyo
Katika uetezi
wake mshitakiwa aliiomba mahakama imwachie huru kwani yeye hakutenda kosa hilo na pia umri wake
bado ni kijana mdogo na wazazi wake bado wanamtegemea maombi ambayo yalipingwa vikari na mwendesha
mashitaka
Hakimu Chiganga
baada ya kusikiliza utetezi huo aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa amehukumiwa na mahakama
baada ya kupatikana na hatia ya kumwingilia kinyume na maumbile
kijana huyo na anahukumiwa na adhabu ya
kifungu cha sheria namba 235 sura ya 20 ya mwaka 2009 hivyo Wiliamu
George mahakama imehukumu kutumikia jela kuanzia jana kifungo cha miaka 30 jela
No comments:
Post a Comment