Saturday, March 8, 2014

DIWANI WA KATA YA ILUNDE AFARIKI DUNIA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Diwani wa Kata ya Ilunde   Halmashauri ya Wilaya ya Mlele  kupitia chama  cha Mapinduzi CCM Filberti Katola 49 amefariki  Duani  hapo juzi  wakati akisafirishwa kurudishwa  kijijini kwake Ilunde
Diwani huyo alifariki juzi  majira ya saa saba mchana  katika eneo la Kanono Wilayani  Mlele  wakati  akiwa njiani  alipokuwa akirudishwa kijijni kwake  baada ya kuwa ametolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda alikokuwa akitibiwa
Marehemu alilazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa zaidi ya wiki mmoja  baada ya kuwa ametokea kwenye hospitali  ya Sikonge iliyoko mkoani Tabara baada ya kuwa anasumbuliwa na maradhi  mbalimbali kwa kipindi kirefu
Ndugu  wa marehemu waliamua  kumuhamisha katika Hospitali ya wilaya ya Mpanda na kumrudisha kijijini kwake kwenye kijiji  cha Ilunde  baada ya kuona hari yake  inazidi kuwa mbaya siku hadi siku licha ya kuwaanapatiwa matibabu
Ndipo hapo juzi wakati wakiwa njiani kwa  kutumia usafiri wa gari  dogo  walifika maeneo ya Kanono Diwani huyo alifariki Dunia
Mazishi ya Diwani Filberti  Katola yamefanyika hapo jana saa saba mchana katika makaburi ya kiji cha Ilunde na huhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Mlele na madiwani wa Halmashari hiyo pamoja na mamia ya wakazi wa Kata ya Ilunde

No comments:

Post a Comment