Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe akishiriki kupanda mbegu shambani.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe Ametoa changamoto kwa wataalam
kuanzisha mashamba darasa katika maeneo yao yatakayotumiwa na wakulima
kujifunza kwa vitendo na kuondokana na dhana kulima kwa mazoea kwa kuwa
kilimo hicho kimepitwa na wakati na hakina tija.
Dkt
Rutengwe alitoa kauli hiyo wakati akishiriki katika shughuli za kilimo
kwenye shamba la mfano lililoko kwenye kijiji cha mwenge kwa
kuwashirikisha watalaam wa kilimo mkoani humo na wananchi wa kata ya
nsimbo kuwaonesha kwa vitendo namna ya kulima kwa kufuata utalaam na
maelekezo wanayopewa na maafisa ugani wa kijiji husika kasha akagiza
kila Afisa ugani katika eneo lake awe na shamba la kujifunza wakulima
ili kile wanachojifunza wakifanyie mazoezi kwenye mashamba yao.
kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Mwenge Kata ya Nsimbo
wameshiriki kwa vitendo katika kutekeleza azima ya kilimo kwanza kwa
vitendo kwa kutoa elimu ya kilimo bora na chenye tija kwa kuwafundisha
wakulima kulima kwa kufuata kanuni bora za kilimo kwa kupanda kwa
mstari, kwa kutumia mbegu bora na mbolea ya minjingu na Inyala
inayotolewa na Kampuni ya Mosanto na mbegu za muda zianzokoma kwa muda
mfupi na mrefu kulingana na hali ya hewa ya eneo husika mbali na kulima
katika shamba lake hilo ambalo amelitoa kwa wananchi kuwa shamba darasa
la kujifunzia pia alishiriki katika zoezi jingine la kupanda shamba la
waziri mkuu Mizengo Pinda lililoko kijijini kwake kibaoni ikiwa nalo ni
shamba la mfano kwa ajili ya kufundishia wakulima mkoani humo na shamba
la kitaifa.
Kwa
upande wake Afisa ugani kutoka SAGOT Joanita Elias alieleza kuwa
Kampuni ya Mosanto ianyouza mbegu za mahindi aina ya DK na mbolea aina
ya Ayara ni kampuni ambayo inatoa mbegu mbole ana mbolea yenye ubora
ambayo inasidia kusitawisha mazao kwa muda mfupi na haina madhara.
Akifafanua
zaidi alieleza kuwa katika zoezi hilo ambalo lilioneshwa namna ya
kupanda kwa msta mahindi ya muda wa kati yanayokoma kwa muda wa siku
120, mahindi ya muda mfupi yanayokoma kwa muda mfupi wa muda siku 90.
pia walipandia mbolea ana ya mijingu inayotengenezwa hapa nchini
Chanzo;Full shangwe
No comments:
Post a Comment